Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wa taasi mbalimbali ambapo amemteua Prof. Abel N. Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI). akichukua nafasi ya Dkt. Respicious Boniface ambaye amemaliza muda wake.

Mbali na Makubi Rais Samia, amemteua Omar Issa kuwa Mkuu (Chancellor) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).
Issa ni Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO na anachukua nafasi ya Mhe. Dkt. Gharib Bilali, Makamu wa Rais Mstaafu ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Taifa cha Ulinzi (NDC).
Dkt. Mzee alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Marten Y. C. Lumbanga aliyemaliza muda wake.
Aidha Rais amemteua Dkt. Edwin Mhede kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Plc kwa kipindi cha pili.

By Jamhuri