Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wageni, viongozi mbalimbali pamoja na Washarika wa Kanisa la Azania Front wakati wa Ibada Maalum ya Kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa iliyofanyika Kanisani hapo Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa mara baada ya Ibada Maalum ya Kumuingiza kazini Askofu huyo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Januari, 2024.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa akizungumza wakati wa Ibada Maalum ya Kumuingiza kazini iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Januari, 2024.