Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Frank Walter Steinmeier Novemba 1, 2023 amewasili Uwanja wa Ndege wa Songea Mkoani Ruvuma kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani hapo.

Rais Dkt. Steinmeier amepokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro, Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

Akiwa mkoani hapo Steinmeier atatembelea Makumbusho ya Mashujaa waliopigana vita ya Majiamaji pamoja na kukutana na familia za waliopigana vita hiyo.