Rais wa Urusi awasili China kujadili vita ya Israel

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amewasili China kukutana na rafiki yake Rais Xi Jinping katika kuimarisha uhusiano wao na kujadili zaidi vita vya Israel na kundi la Palestina la Hamas, mtandao wa India Today umeeleza.

China wiki hii inakaribisha wawakilishi wa nchi 130 kwa ajili ya kongamano la mradi wa kihistoria wa Rais Xi, Mpango wa Belt na Road, ambao Beijing inatumia kupanua ushawishi wake duniani.

Putin ni miongoni mwa waalikwa, huku kiongozi huyo wa Urusi akiwa katika safari yake ya kwanza kwenye nchi yenye nguvu kubwa duniani tangu uvamizi wa Ukraine.

“Anatarajiwa kukutana na Xi kwa mazungumzo Jumatano, “ taarifa ya Ikulu ya Kremlin Urusi ilisema,”

“Wakati wa mazungumzo, umakini maalum utatolewa kwa masuala ya kimataifa na kikanda.” ilisema, bila kufafanua.

Taarifa hiyo imeeleza Putin yuko kwenye dhamira ya kuimarisha uhusiano ulio na nguvu ingawa Moscow inazidi kuwa mshirika mdogo.