Na Helena Magabe, JamhuriMedia, Tarime

Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanda amewapongeza askari wanawake toka Kanda maalumu Tarime/Rorya kwa kuheshimisha Siku ya Wanawake.

Akizungumza katika maadhimisho ambayo kimkoa yamefanyikia katika Kata ya Nyamswa wilayani Bunda amesema hawajawahi kushindwa kusherehesha.

Askari hao ambao walikuwa na bango lao kubwa wakifurahia siku ya wanawake walikuwa kivutio na kuonyesha kufurahia zaidi siku ya Mwanamke ambapo Kauli mbiu ilikuwa ni Wekeza kwa Mwanamke kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa Jamii.

Mtanda amewataka wanaume wa Mkoa wa Mara na Simuyu kuwapa Wanawake fursa ya kujipambanua na kuwajengea uwezo wa kujitegemea kutafuta ili watapokuwa wamefariki wanawake wajisimamie.

Amesema kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2020 inaonyesha asilimia 33 ya Wanawake wa Mara na Simuyu ndio wanaotunza familia zao.

Aidha amesema Wanawake wasifanywe wategemezi watumie fursa za mikopo katika Benki zisizo na riba na kukopa kwenye Halmashauri pesa za Serikali

Aidha amesema shilingi Bilioni 2 zilitolewa na Serikali kwenye Halmashauri za Mkoa Mara ili kukopesha vikundi vya kijamii na kwamba shilingi milioni 778 zitatolewa kwa wanawake utaratibu wa serikali ukikamilika ili wakopeshwe na riba yake ni asilimia 10

Wanawake wakakope na kuondokana na mikopo ya kausha damu,mikopo umiza na migineyo mingi inyopelekea matatizo makubwa kwenye familia zao .

Amempongeza Neema Ibanda Afisa maendeleo ya jamii mkoa Mara pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bunda kwa maandalizi mazuri ya siku ya wanawake pamoja na Waandishi wa Habari kwa kuibua habari za ukatili.

Hata hivyo amewaomba Wanawake kujitokeza kugombea katika nafasi mbali mbali na kuwasihi Wanawake wa vyama vyote kumpigia kura Rais Mhe Mama Samia Suluhu Hasan kura 2025.

” Ninawaomba Wanawake wa vyama vyote muungane kumpigia Mama Samia kura 2025 mmtie moyo adui wawanamke si mwanamke ni kushirikiana na sisi hatukakuwa tayari kuona mama anadhihakiwa kwa jinsia yake” alisema Mtanda

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Vincent Naano amesema hakuna maendeleo bila Mwanamke na ukatili bado upo Mara.

Amesema maendeleo yoyote yanachangiwa na Wanawake hivyo ni vema Wanawake wakashirikishwa vema kwenye maendelea.

” Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ukatili bado upo hata jana kuna Mama alikamatwa amefungia watoto mapacha wasiende shule” alisema Naano

Diwani ya kata ya Nyamswa ameiomba Jamii kuwapenda Wanawake na kusema kuwa yeye anawapenda sana Wanawake na wanastahili upendo.

Iakini amewataka Wanawake kushiriki vema kwenye malezi ya watoto na sio kuwaachia wanaume sambamba na kuwahisi Wanawake kuacha tabia ya kuwachonganisha watoto na baba zao.

Amesema kabla hajawa Diwani alikuwa dereva kwenye kituo kimoja cha afya alikuwa akiona kina Mama walivyokuwa wakiteseka kupata huduma ya kujifungua ndio maana anawapenda na hakuna binadamu ambaye hakuzaliwa na Mama.

Amina Hoza ni Mkaguzi Msaidizi Wilaya ya kipolisi Tarime/ Rorya ambaye yuko kwenye kitengo cha Dawati la jinsia yeye ana laani vikali baadhi ya watoto wanadanganywa kwa kigezo kuwa wanapelekwa shule kusoma badala yake kunageuzwa watumishi wa kazi za ndani.

Akizungumza kwa hisia Kali amesema anachukia sana na kulaani kitendo cha baadhi ya watu wakimemo Walimu kuwachukua watoto kwa Wazazi wao kwa
makubaliano ya kuwasaidia kuwasomeshea Watoto wao wa kike kumbe lengo ni kuwatumikisha.

Amesema kuwa kuna ulazima gani kumchukua mtoto mwenye wazazi wake kuwa anaenda kumsomeshwa wakati ana wazazi wake ni vema amsomeshe akiwa kwa wazazi wake kwani wanapowachukua makubaliano ni masomo na si vinginevyo.

Hoza amesema anekutana na kesi nyingi za hivyo hivi karibuni alimwokoa binti wa kidato cha kwanza kutoka kwa Mwalimu mmoja wa shule ya mazoezi Buhemba .

“Nitazunguka shule zote nafanya mikutano na Walimu nikimkuta Mwalimu mwenye mtoto ana kesi ya kujibu wanachukua watoto eti wanaenda kuwasomesha kumbe wanaenda kuwafanyisha kazi za kufua kulea watoto na kupika hawapati hata muda wa kujisomea” alisema Hoza.

Mkurugenzi wa Shirika la Tumaini la Msichana na Mwanamke Tanzania (Hope for Girls and Women Tanzania) na Mjumbe wa Baraza kuu CCM Taifa Rhobi Samweli amesema kupitia maadhimisho hayo Wanawake wengi wataiga mfano wa Wenzao kama alivyojionea kwa Polisi Wanawake ,madini,Takukuru pamoja na sekta nyingine.

Amesema anaungana na Mkuu wa Mkoa Said Mtanda pamoja na Mwenyekiti wa UWT Mkoa Nancy Msafiri kuwaomba Wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.

Amesema yeye kama mdau wa maendeleo anaamini maadhimisho ya mwaka huu yataleta mwamko mkubwa kwenye Jamii yetu ambapo kwa Mwaka Kesho kutakuwa na mabadiriko makubwa kwani mwanamke ndie anajua umuhimu shule kuwa karibu ndie anajua umuhimu wa Hosptali na mambo mengi hivyo
mwanamke akiwa Kiongozi atafanya maendeleo mengi kwenye Jamii.

Aidha ametoa wito Wanawake wajitokeze kujiunga kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali kwani wakijiunga katika sekta hizo wakawa wengi watasaidia kuharakisha maendeleo .

Aidha amesema yeye ni mwanahakati mpambanaji dhidi ya ukatili na anaendelea na harakati na kuiomba Jamii kuungana kwa pamoja kupinga ukatili kwa Watoto na Wanawake.