Na Isri Mohamed

Mahakama kuu Kanda ya Manyara, imepanga kusikiliza rufaa ya tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Babati mjini Paulina Gekul, za kumshambulia Hashimu Ally, Machi 21,2024, Chini ya jaji wa mahakama hiyo Devotha Kamzora.

Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Manyara, Devotha Kamzora amesoma tarehe ya kusikiliza shauri hilo na kusema kumbukumbu za mahakama hazioneshi kama upande wa Gekul au mawakili wake walipata wito wa Mahakama chini ya kifungu Cha 101 CPA.

Hivyo kutoa haki upande wa Gekul kupata nafasi ya kusoma rufaa hiyo na kuweza kujibu.

Hashimu Ally aliwakilishwa na mawakili wake watatu wakiongozwa na wakili Peter Madeleka, Huku upande wa Gekul ukiwakilishwa na mawakili wakiongozwa na Efraimu Kisanga.

By Jamhuri