Dkt.William Ruto ameapishwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Kenya leo Jumanne Septemba 13,2022 katika uwanja wa Karasani jijini Nairobi.

Ruto ameapishwa na Jaji Mkuu Martha Koome kuchukua nafasi ya Uhuru Kenyatta,ambaye amemaliza muda wake wa utawala wa miaka kumi.

Ruto alikuwa Naibu wa Rais,anaanza safari ya kuwaongoza Wakenya ,baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 19,2022 kwa kumshinda Raila Odinga mwenye miaka 77.