Serengeti Boys yatinga nusu fainali CECAFA

TIMU ya taifa ya Tanzania imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano ya CECAFA U17 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Somalia jana Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mabao ya Serengeti Boys katika mchezo huo wa mwisho wa Kundi A yote yamefungwa na Sylvester Otto dakika ya 75 na 80 na kwa matokeo hayo wanamaliza na pointi sita kufuatia awali kuwafunga wenyeji, Ethiopia 3-2.