Na Mwandishi Wetu

Serikali imepiga marufuku shule za bweni kwa wanafunzi wa shule ya awali na madarasa ya mwanzo ya shule za msingi , malengo ni kuwapa watoto fursa ya kuwa na uhusiano na familia zao kuelewa mila, tamaduni na maadili ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Elimu Lyabwene Mtahabwa alisema kuwa huduma za bweni kwa watoto wenye hadi umri wa hadi miaka 10 zitamalizika mwezi ujao, na wataendelea kuwa wanafunzi wa kutwa hadi watakapofika darasa la tano.

Pia hairuhusiwi kwa shule yoyote ile kuwa na makambi ya kitaalum. Hatua hii inaakisi utekelezaji wa Waraka wa Elimu No.3 wa mwaka 2007 kuhusu Kukataza Kambu za masomo kwa shule za msingi.

Amesema vizuizi vinaweza kutotekelezwa kwa wanafunzi ambao wazazi wao au walezi watapata kibali maalum cha kuwaepusha na mabadiliko ya sheria.

Mtahabwa amesema shule yoyote itakayobainika kukiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua za kinidhamu.

By Jamhuri