Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia,Dodoma

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ameuagiza Wakala wa Vipimo (WMA) kuwashughulikia wafanyabiashara wanao wanyonya wakulima kwa kutumia ujazo uliopitiliza unaojulikana kama lumbesa na kueleza kuwa kipimo hicho ni mwiba kwa wakulima unaiwasababishia umaskini.

Hayo yameelewa leo February 6,2024 Jijini hapa kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa jengo la makao mkuu ya wakala huo nchini na kueleza kuwa tatizo hilo limekuwa la muda mrefu na wakulima nchini wamekuwa wakilalamika mara nyingi lakini bado linajirudi.

Waziri Majaliwa amefafanua kuwa licha ya wakulima kutumia nguvu nyingi kwenye kilimo bado wanaishia kuwa masikini kutokana na juhudi zao kukatishwa kwenye kipimo cha lumbesa na hivyo kuutaka wakala huo kulifuatilia kwa ukaribu suala hilo na kutolea mfano kwamba kama mtu anataka vitunguu kilo 100 basi apate kilo hizo na kifungashio kiwe cha ujazo huo huo na siyo vinginevyo.

“Wafanyabishara nchini hakikisheni mnazingatia vipimo na kuacha tabia ya kujinufaisha kwa kuwaibia wengine, acheni kulegeza vipimo vilivyowekwa, acheni kuwaibia wengine na wanachi tunabidi kuwa wajanja kila tumapohitaji bidhaa lazima kuzingatia ujazo kwa mujibu wa vipimo vilivyowekwa kisheria”amesema

Amesema Watumishi wa wakala huo wanapaswa kusimamia vyema sheria pamoja kanuni zake na kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa vipimo mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ili kukomesha tabia hiyo.

Kuhusu ujenzi wa jengo hilo Majaliwa ametumia nafasi hiyo kuipongeza WMA, kwa kutekeleza maagizo ya serikali ya taasisi zote za umma kuwa na ofisi makao makuu ya nchi kwa kuwa na jengo la kisasa linaloendana na hadhi ya makao makuu huku akiwatahadharisha kuwa ujenzi huo unapaswa kuendana na thamani ya fedha.

Amesisitiza kuwa, “Katika hili naziagiza taasisi nyingine kuhakikisha kuwa wanatekeleza maelekezo haya ili kuipunguzia mzigo serikali wa fedha kwa ajili ya kupanga nyumba za ofisi”amesema

Pamoja na hayo Waziri Mkuu ameizungumzia, ujenzi wa Mji wa kiserikali uliopo eneo la Mtumba ambao umeanza kwa awamu ya pili kuwa umefikia asilimia 73.4 kwa majengo yote 29 ambayo yanajengwa kwa sasa na kwamna zipo wizara ambazo ujenzi wa majengo yake umefikia asilimia zaidi ya 90.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biasha Dk. Ashatu Kijaji, alisema kuhusu sula la matumizi ya lumbesa tayari serikali imeshaunda Tume ambayo inafanyia kazi jambo hilo na itakuja na majabu nama bora ya kulimaliza.

Amesema kwa sasa ipo tume ambayo inafanyia kazi suala la lumbesa na itakuja na majibu ili kabla ya mwaka mpya wa fedha kuanza Serikali tutatoa maagizo kwa mujibu wa sheria ya fedha kuhusu lumbesa.

Akizungumza kuhusu jengo hilo alisema limefikia asilimia 70.34 na tayari kiasi cha Sh. bilioni 3.25 kati ya bilioni 6.73 zinazohitajika katika kukamilisha mradi huo.

By Jamhuri