Wachezaji wa Kikosi cha Simba Sc wakishangilia goli wakiwa katika mchezo wa kirafiki wa kuhitimisha Tamasha la 16 la Simba DAY uliopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Agosti 3, 2024, Dar es Salaam, katika mchezo huo wamefanikiwa kuibuka na  ushindi wa mbao 2 -0 dhidi ya APR ya Rwanda 

……. 

Wekundu wa Msimbazi Simba Sc wamefanikia kuibuka na ushindi wa mbao 2 -0 dhidi ya APR ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kuhitimisha tamasha la 16 la Simba DAY uliopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Agosti 3, 2024, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba Sc yamefungwa na kiungo wao mpya Debora Fernandez Mavambo mwenye uraia pacha wa Kongo Brazaville pamoja na Angola katika dakika ya 46.

Huku bao la pili likifungwa na Mshambuliaji Edwin Charles Balua dakika 66, huu ni mchezo wan ne mfululizo Simba Sc inashinda chini ya kocha mpya Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids.

Katika tamasha hilo mashabiki wa Simba Sc walijiokeza kwa idadi kubwa na kuujaza uwanja wa Benjamini Mkapa, ambapo tukio hilo liliambatana na utambulisho wa kikosi kipya cha timu hiyo ambacho kitashiriki michuano ya msimu wa 2024/2025.

Please follow and like us:
Pin Share