Watu wanaweza kusema hakuna stendi Tabata Kimanga kwani kinachoonekana pale ni dampo la uchafu. Diwani na Serikali ya Mtaa tusaidiane.

Fakhii Mohamedy, 0673774241

Serikali isiue demokrasia 

Ombi langu kwa Serikali yetu ya Awamu ya Tano ione uwepo wa vyama vya upinzani nchini ni moja ya njia ya kuikosoa serikali pale inapokosea kutekeleza masuala muhimu ya wananchi.

Kayai Mdoe, Kiteto, Manyara 0629046430

NEMC mje Kivule

NEMC waje Kivule Frem kumi na Minazini kwa Nyahili washughulikie uchafuzi wa mazingira wa sauti (sound pollution) unaofanywa na makanisa. Wananchi hawawezi kupumzika jioni na asubuhi wanaamshwa na vipaza sauti.

Msomaji wa JAMHURI, 0682874626 

Masasi Mlingula hatuna maji

Sisi wakazi wa Masasi Mlingula kwa muda mrefu hatuna maji. Tunakuomba Rais John Magufuli tusaidie, kwani tunateseka sana.

Msomaji wa JAMHURI, Masasi 0683764221

Tunahitaji maji Ubungo, Goba

kero yangu ni kuhusu maji. Sisi wakazi wa Goba Wilaya ya Ubungo hatuna maji ya bomba tunakunywa maji ya visima, Serikali ituangalie kwa jicho la pili.

Msomaji wa JAMHURI, Ubungo, Goba 0673721215

Mheshimiwa Rais nisaidie

Mheshimiwa Rais Magufuli mimi mlemavu wa miguu kutoka mkoani Tabora kwa muda mrefu nimemwomba Waziri mwenye dhamani anisaidie kutatua kero yangu lakini ameshindwa naomba nikuone unisaidie.

Msomaji wa JAMHURI, Tabora  0685782894

Takukuru msilale usingizi

Wakati umefika kwa uongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa hapa nchini (Takukuru), kutupia macho tatizo la ufisadi katika ofisi za Umma. Nasema watupie macho kwa sababu tumeona vitendo vya ubadhilifu wa mali za wanyonge.

Salim Liundi, 0659601205

Matosa tunahitaji shule ya msingi

Nikiwa kama mkazi wa eneo la Matosa na mpenda elimu na maendeleo kwa ujumla, naomba kuwazindua viongozi wetu kuanzia ngazi ya kijiji mpaka taifa, kuwa hapa matosa hakuna shule ya msingi,iliyopo ni ya Sekondari tu na hatuoni jitihada zozote za kutatua kero hii.

Msomaji wa JAMHURI, Kimara Matosa, Dar es Salaam 0712184111

Serikali ipige marufuku kubet

Serikali iliwahi kupiga marufuku michezo ya Pool nyakati za asubuhi ili vijana wasibweteke na badala yake wautumie muda huo kwa kutafuta elimu na kufanya kazi. Sasa igeukie kamari, inayojulikana kama Sportsbetting.

Msomaji wa JAMHURI, 0754356333

Hongera JAMHURI

Hongera gazeti la JAMHURI kwa kutumulikia wanyonge na sauti zetu kusikika. Hoja yangu leo nikiwa kama mjasiliamali mnifikishie ombi langu kwa mheshimiwa Rais ili anidhamini mkopo wa basi aina ya Coaster nitafanya marejesho kwa uaminifu mkubwa.

Frank lehani, Kimara Dar es Salaam, 0716949484

Tanroads, Manispaa mkarabati mifereji

Tanroads na Manispaa mifereji ya maji barabarani haikarabatiwi na matokeo yake kujaa michanga na uchafu, barabara kuharibika mapema na kusababisha mafuriko. Anzisheni kitengo maalumu kusimamia mifereji katika barabara zote na hiyo itaokoa fedha za umma.

John Baptist, 0784967862

Ukaguzi wa majengo

Nakumbuka miaka michache iliyopita Serikali ilifanya ukaguzi wa majengo katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Kariakoo baada ya jengo moja lililojengwa chini ya viwango kuporomoka na kusababisha maafa. Katika ukaguzi huo majengo mengi yalionekana yamejengwa chini ya viwango. Sasa kama yamefanyiwa marekebisho tujulishwe kwani hakuna kilichoendelea baada ya ukaguzi huo.

Shirima, Morogoro 0755549720

TANESCO acheni ubabaishaji

Mimi ni mwanachi kutoka Wilaya ya Karatu, kero yangu ni kuhusu Shirika la Umeme (Tanesco), wameweka nguzo katikati ya kiwanja changu na kupitisha nyaya za umeme juu ya nyumba yangu; nikiwauliza wanasema suala hilo linamuhusu aliyeingiza umeme, naye anapoulizwa anasema niwaulize Tanesco. Sielewi nifanyeje?

Msomaji wa JAMHURI, Karatu 0755186724

Maadili ya vijana

Watanzania tuamke kwani maadili ya vijana wa taifa yametoweka. Nasema hivi kwa kuwa tumeona makundi mengi ya vijana wakijiingiza katika vijiwe vya wahuni na kutumia dawa za kulevya kwa kuwa hawana njia mbadala ya kujikwamua kiuchumi na maisha ya familia zao. Taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s) zisaidie ili kumaliza wingi wa vijana wanaokaa mitaani bila kuwa na shughuli maalumu.

Salim Liundi, 0659601205

Biashara ya bangi

Pamoja na kupigwa marufuku kwa biashara ya bangi na dawa zingine za kulevya, bangi inaendelea kuuzwa mitaani hadharani na kuvutwa hadharani tena mbele ya mabanda ya vyakula vya mama lishe. Polisi kazeni buti kutokomeza uovu huu uliokithiri hapa Dar es Salaam, kwa kuwa nguvu kazi ya inapotea kwa vijana hawa kuendelea kuvuta bangi na dawa za kulevya.

Msomaji wa JAMHURI, 0764209404

 

 

4527 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!