Kutokana na kukithiri kwa madeni ya muda mrefu katika sekta ya Ardhi Serikali imezitaka Taasisi za umma na binafsi nchini kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi ya pango la ardhi ndani ya mwezi mmoja kwani jambo hilo limekuwa ni changamoto kubwa katika sekta hiyo.

Hayo yamesemwa Leo jijini Arusha na Katibu mkuu wa wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,Dk Allan Kijazi wakati akifungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mkakati wa makusanyo ya kodi ya pango la ardhi kwa kushirikiana na benki ya CRDB.

Dk. Kijazi amesema kuwa,taasisi za umma zinazoongoza kwa malimbikizo ya kodi nchini hivyo ifikapo desemba 31 mwaka huu wawe wameshalipa.

“Katika maeneo ambayo yanaturudisha nyuma kwenye ukusanyaji wa kodi ni mashirika ya umma kupitia wizara mbalimbali na serikali za mitaa wao huchukulia hawawajibiki kulipa kodi ya ardhi na tozo mbalimbali za serikali,”amesema Dk Kijazi.

Dk.Kijazi amesema taasisi hizo za umma zimelimbikiza madeni ya kodi ya ardhi takribani sh 70 bilioni hivyo anasisitiza wahusika wote kutii sheria bila shuruti.

Kamishna wa ardhi nchini,Mathew Nhonge amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 wanamalengo ya kukusanya takribani sh 250.1 bilioni ambapo moja ya mikakati ni kupeleka ankara kwa wamiliki wa viwanja na wanaposhindwa wanachukuliwa hatua za kisheria.

“Mara nyingi tumekuwa tukitumia vituo vyetu vya makusanyo kupitia Ofisi za ardhi za mikoa, pamoja na halmashauri zote nchini lakini pamoja na hilo kwa sasa tumeona kushirikiana na taasisi nyingine zenye mtandao mkubwa,”amesema.

Mwakilishi wa Benki ya CRDB,Gerald Kamugisha amesema wako tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha makusanyo ya serikali yanakusanywa kikamilifu na kupunguza gharama za mwananchi kufikia