Wahariri wa vyombo vya habari nchini kupitia Jukwaa la wahariri wamepigwa na tabasamu baada ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro na kushuhudia maajabu yenye simulizi mnato.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deodatus Balile wahariri hao walielezwa kuhusu uthibitisho wa kisayansi unaodhihirisha kuwa binadamu wa kale alipatikana katika bonde la Olduvai.

Maajabu mengine waliyopata simulizi yake ni mchanga wa kunogesha mahaba ama mchanga unaohama ambao pamoja na mambo mengine ni sehemu pekee ya kuimarisha upendo hasa mahaba yaliyolegalega.

Wahariri wa vyombo vya habari nchini kupitia Jukwaa la wahariri wamepigwa na tabasamu baada ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro na kushuhudia maajabu yenye simulizi mnato.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deodatus Balile wahariri hao walielezwa kuhusu uthibitisho wa kisayansi unsodhihirisha kuwa binadamu wa kale alipatikana katika bonde la Olduvai.

Maajabu mengine waliyopata simulizi yake ni mchanga wa kunogesha mahaba ama mchanga unaohama ambao pamoja na mambo mengine ni sehemu pekee ya kuimarisha upendo hasa mahaba yaliyolegalega.

Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Dkt.Abdul-Razaq Badru amewaeleza wahariri hao kuwa Hifadhi ya Ngorongoro ina mvuto mkubwa kutokana na uwezo wake wa vivutio na Urithi wa utamaduni.

Kamishna Dkt. Badruamewaeleza wahariri hao kuwa katika kuelekea Mashindano ya AFCON mwaka 2027, Ngorongoro imejipanga kikamilifu kupokea wageni wakaokuja kutalii ambapo kwa sasa nguvu kubwa ni kuboresha miundombinu ya utalii kuimarisha mifumo ya malipo, ujenzi wa barabara kutoka geti la Loduare hadi Seneto km 29.5 kwa tabaka gumu sambamba na kuimarisha kivutio cha maporomoko ya maji Endoro ambapo ujenzi wa ofisi za kisasa za kutolea huduma na njia za watembea kwa miguu zinajengwa katika eneo hilo.

Akiongea kwa niaba ya Wahariri, Mwenyekiti wa jukwaa wa Wahariri Deodatus Balile ameeleza kuwa Ngorongoro ni mdau muhimu katika kuchangia pato la taifa na huduma za wananchi kupitia mapato ya utalii na kusema kuwa jukwaa hilo litaendelea kushauri kwa karibu kuhusu hifadhi hiyo.