Na Magrethy Katengu, JamuhuriMedia, Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeaminiwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ambapo katika maadhimisho hayo ya miaka 20 tanayotarajiwa kufanyika Mei 25,2024 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa kimataifa ambapo mwenyekiti wa Mkutano huo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .

Tanzani kuwa nchi mwenyeji imepewa jukumu kubwa la kusimamia shughuli zote zinahusu Baraza, ikiwemo kufuatilia kwa karibu hali ya ulinzi na usalama kwenye Bara la Afrika kutoa miongozo ya kushughulikia masuala ya kiusalama pale inabidi; na pia kuandaa ratiba na kuongoza vikao vya Baraza.

Amebainisha hayo leo Mei 22 ,2024 Jijini Dar es salaam Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba amesema Hayo ni majukumu makubwa; na bila shaka Tanzania kuaminiwa na kukabidhiwa ni kutokana na heshima kubwa iliyonayo Barani Afrika na duniani hivyo fursa hiyo ni kumshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuimarisha Diplomasia ya nchi na kuiongoza kutoa kipaumbele kwenye masuala ya ulinzi na usalama katika Bara la Afrika na duniani .

Waziri Makamba amefafanua kuwa mwezi Machi mwaka 2022, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilichaguliwa kuhudumu kwenye nafasi ya Mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kwa miaka miwili hadi mwezi Machi 2024 ambapo muda wa kuhudumu ulifikia kikomo hivyo Wakati wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Mkutano wa Baraza la Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Februari 2024 Jijini Adiss Ababa, Ethiopia Tanzania ilichaguliwa tena kuhudumu kwenye Baraza hilo kwa muhula mwingine wa miaka miwili hadi mwaka 2026.

” Baraza la Amani na Usalama ni chombo cha juu kabisa cha maamuzi kuhusu masuala ya amani na usalama kwenye Umoja wa Afrika miongoni mwa majukumu ya Baraza hili ni kuzuia kutokea kwa migogoro,kusuluhisha au kukabiliana nayo pale inapojitokeza, baraza hili lilianzishwa mwaka 2004 kuchukua nafasi ya Chombo cha Kuzuia na Kukabiliana na Migogoro (Central Organ for Conflict Prevention and Management) uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (Organization of African Unity – OAU)”amesema Waziri

Waziri Makamba amesema mchi 15 tu kati ya nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika ndio Wajumbe wanaounda Baraza hilo na kwa sasa nchi hizo 15 ndiyo wajumbe ikiwemo Tanzania, Uganda na Djibouti (kutoka Ukanda wa Mashariki); Cameroon, DRC na Equatorial Guinea (Kanda ya Kati); Afrika Kusini, Angola na Botswana (Kanda ya Kusini); Cote d’Ivoire, Gambia, Nigeria na Sierra Leone (Magharibi) na;Misri na Morocco (Ukanda wa Kaskazini).

Sanjari na hayo Tanzania kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Baraza wameandaa ratiba ya shughuli mbalimbali kwanza, walikubaliana na kila wiki katika mwezi huu waipe dhima yake mahsusi na Wiki ya kwanza itahusu usuluhishi na majadiliano (mediation and dialogue), ya pili ilihusu masuala ya mahitaji ya kibinadamu, amani na usalama (humanitarian, peace and security), ya tatu ilihusu wanawake na vijana katika amani na usalama (women and youth, peace and security),ya nne ulinzi kwa watoto (child protection) , ya tano ilihusu kusaidia misheni za amani (peace support operations).

“Ni ukweli usiopinga kuwa katika kipindi cha miaka 20 ya uhai wake, Baraza limepata mafanikio katika kuimarisha amani na usalama Barani Afrika Migogoro mingi imepata ufumbuzi (Burundi, Comoro, Madagascar, Cote d’Ivoire, Liberia, Sierra Leone) hata hivyo, changamoto bado zipo, ikiwemo kuendelea kwa migogoro ya muda mrefu ya Somalia, DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Libya na Sudan hivyo Maadhimisho haya yanatoa fursa kwa Waafrika wote na watu wote wenye kuitakia mema Afrika kutoa maoni yao ya kuliimarisha Baraza ili liweze kushughulikia changamoto za kiusalama ” amesema Waziri

Aidha Maadhimisho hayo yataongozwa ;Kaulimbiu ni; “Miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ikiwa Chombo cha Maamuzi” na yanatarajiwa kuhudhuriwa na wageni takriban 120 kutoka nchi mbalimbali na Miongoni mwa watu mashuhuri watakaoshiriki ni pamoja na Mhe. Jessica Alupo, Makamu Rais wa Uganda; Mhe. Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika; Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Olesegun Obasanjo; Rais Mstaafu Burundi, Mhe. Domitien Ndayizeye; Rais Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Joachim Chissano na Mhe. Rais wetu Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kwa hapa nchini, wamealikwa takriban washiriki 700 hivyo Watanzania hatuna budi kujiandaa kupokea ugeni huo mkubwa.