Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media, Dubai

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo imetia saini Mkataba wa Makubaliano (MOU) na Ofisi ya Mwanafamilia ya Kifalme ya Dubai Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum, ili kutoa usambazaji wa kimkakati na uhifadhi wa mbolea nchini kwa usalama wa chakula.

Mkataba huo umesainiwa leo Februari 25,2023 baina ya Wizara ya Kilimo pamoja na Ofisi hiyo ya kibinafsi, ambapo makubaliano hayo yanaeleza dhamira ya kutoa mbolea ya uhakika na thabiti kwa Tanzania, ambayo itasaidia sekta ya kilimo nchini na kuboresha usalama wa chakula.

Chini ya masharti ya makubaliano hayo, Ofisi hiyo ya Kibinafsi pamoja na washirika wake itaendeleza na kuendesha kituo cha kisasa cha kuhifadhi mbolea nchini Tanzania, ambacho kitakuwa na uwezo wa kuhimili usambazaji wa kimkakati wa bidhaa za mbolea.

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Hussein Mohamed Bashe, akiteta jambo na Mwanafamilia ya Kifalme Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum. PICHA | OFISI YA KIBINAFSI YA SHEIK MAKTOUM

Serikali itawezesha kutoa miundombinu iliyopo katika maeneo tarajiwa. Kituo hicho kitawekwa kimkakati ili kuhakikisha kuwa wakulima kote nchini wanapata mahitaji ya mbolea kwa bei shindani.

Serikali ya Tanzania imekubali kupunguza kiasi cha mbolea kwa ajili ya kusambazwa kwa wakulima kote nchini.

Ushirikiano huu utasaidia kuhakikisha wakulima wa Tanzania wanapata mbolea ya hali ya juu ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa mazao na mafanikio ya sekta ya kilimo kwa ujumla.

“Tuna furaha kubwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kusaidia sekta ya kilimo nchini.” amesema Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum

“MOU hii inawakilisha hatua kubwa ya maendeleo katika juhudi zetu za kuwapatia wakulima nchini Tanzania mbolea ya hali ya juu wanayohitaji ili kukuza mazao yenye afya na kuboresha maisha yao.” amesema

Ushirikiano huu wa kimkakati kati ya Tanzania na Dubai utasaidia kukuza uchumi, kuboresha usalama wa chakula, na kukuza mazoea ya kilimo endelevu nchini. Ofisi Binafsi imedhamiria kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha mpango huu unafanikiwa na inatarajia ushirikiano wa muda mrefu na wenye tija.

By Jamhuri