Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akiongozana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapologwe pamoja na Timu ya Wataalam wamefanya tathmini ya anga kuona athari ya mafuriko ya matope na mawe jinsi zilivyoathiri huduma za afya mazingira katika mji wa Kateshi Wilaya ya Hanang. Mafuriko hayo yameleta athari na kusababisha vifo vya watu, majeruhi na kuharibu miundombinu ya huduma.