Wajumbe bodi ya JKCI wakutana jijini Dar

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina ambaye pia ni Mratibu wa huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto  Mkoa wa Rukwa akiongoza kikao cha tano cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI  Dkt. Peter Kisenge.

 Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge akitoa taarifa ya utendaji wa kazi zilizofanywa na taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba katika mwaka wa fedha wa 2023/24 wakati wa kikao cha tano cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Viongozi wa Menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi  hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akitoa taarifa ya utendaji wa kazi zilizofanywa na taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba katika mwaka wa fedha wa 2023/24 wakati wa kikao cha tano cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akichangia mada wakati wa kikao cha tano cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni  jijini Dar es Salaam. Kulia ni mjumbe wa Bodi hiyo CPA.Godfrey Kilenga ambaye pia ni Mtendaji Mkuu kutoka ofisi ya TAB Consult Audit Firm Partner.