Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar ea Salaam

Tume ya Habari na Mawasiliano nchini (TEHAMA), imeendaa jukwaa la tatu la usalama wa mitandao ya kielekitroniki la mwaka 2024 litakalofanyika kuanzia April 4 hadi 5 mwaka huu jijini Arusha ambapo washiriki 300 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki.

Akizungumza na wanahabari leo Machi 14, 2024 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa tume hiyo,Dkt Nkundwe Moses mwasaga amesema kongamano hilo litashirikisha jumla ya washiriki na wadau mbalimbali zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi likiwa na lengo la kupitia ajenda kuu tano ndani ya mkutano huo.

Nkundwe amesema wao kama nchi wenyeji wameamua kutoa ufadhili kwa washiriki wanawake 100 watakaolipiwa gharama zote za ushiriki wa kongamano hilo ili kuwapa motisha kushiriki kwenye masuala ya usalama wa kimtandao.

Aidha Nkundwe amewataja baadhi ya wadau watakaoshiriki kongamano hilo kuwa ni pamoja na wale wanaojishughulisha na kutengeneza tafiti, kuelimisha na kusimamia, kuandaa miongozo mbalimbali ya matumizi Salama ya mitandao ya kompyuta na matumizi ya kielekroniki kwa hapa nchini.

Katika hatuna nyingine Nkundwe amesema sababu za kuandaa kongamano hilo hi ni kuangalia zaidi masuala ya kimtandao ikiwemo matumizi ya fedha na haki za mtu binafsi pia kuzuia mashambulizi ya maswala ya kielekroniki na mitandao ya nchi kiusalama.

Aidha mkurugenzi huyo ametaja ajenda kuu tano za mkutano huo kuwa ni (1) kuratibu sera ya tehama (ii) kufanya mageuzi ya kidigitali na kuwapa ujuzi watanzania kuhusu maswala ya tehama.

Aidha pia madhumuni mengine ya mkutano huo ni pamoja na kutoa huduma ya mawasiliano ambayo ni jumuishi kwa makundi yote bila kubagua jinsia.

Katika hatua nyingine Nkundwe ametaja ajenda nyingine ya mkutano huo ni kuwa ni pamoja na kuzuia ushawishi wa makosa ya kimtandao ambayo yanafanywa na watu bila kujua kuwa kufanya hivyo ni makosa kisheria.

Amesema kwa mujibu wa takwimu za kidunia Tanzania Inashika nafasi ya pili kwa usalama wa kimtandao huku nchi ya Mauritius ikiwa ndio kinara kwenye usalama wa maswala ya makosa ya kimtandao na kielekroniki duniani.

Aidha ametoa wito kwa wananchi na wadau wengine kujitokeza kushiriki kongamano Hilo kwani linamanufaa kiuchumi na kijamiii kwa mtu Mmoja Mmoja na Taifa kwa ujumla.

Amesema kutokana na sifa ya kuwa nchi ya pili kiusalama kimtandao wawekezaji wengi kutoka mataifa mbali mbali yameonyesha Nia ya kuja kuwekeza nchini huku akitoa tahadhari kuwa nchi yoyote isiyokuwa na usalama wa mitandao wawekezaji hawawezi kuwekeza mitaji kwa sababu za kiusalama.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo ametaja gharama na ada ya ushiriki wa kongamano la mwaka 2024 kuwa ni shilingi 250,000 kwa wataalamu wa tehama waliosajiliwa na tume ya hiyo na wale wasiosajiliwa watalipia shilingi 300,000 kwa ushiriki wao.

Tume ya TEHAMA ni taasisi yenye jukumu la kukuza na kuendeleza maendeleo ya TEHAMA hapa nchini, inawajibu wa kutathmini utekelezaji wa mikakati mbali mbali na kutoa ushahuri pamoja na muelekeo wa wa utekelezaji wake.

By Jamhuri