Rais Donald Trump amesema anatarajia vita kati ya nchi yake Marekani na Iran kumalizika baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa mwezi Novemba.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano, Trump amesema anaamini vita hivyo vitaisha mara baada ya uchaguzi ujao wa Marekani akidai kuwa wahusika wa mgogoro huo hawawezi kuuendeleza kwa muda mrefu zaidi.
Trump pia ametoa onyo kwa Iran kuhusu eneo la Mlima wa Pickaxe, ambalo linaaminika kuwa na miundombinu ya chini ya ardhi karibu na kituo cha urutubishaji wa urani cha Natanz.
Amesema wanafahamu kikamlifu kuhusu kinachoendelea.
”Tumegundua kuna shughuli fulani zinazoendelea katika eneo la Pickaxe. Ningeishauri Iran isijaribu kufanya uchokozi wowote kwasabu tutalazimika kuishambulia kwa nguvu kubwa sana”
Trump amekuwa akitoa vitisho vya kulishambulia eneo hilo tangu katikati ya mwezi Julai.
Rais huyo wa Marekani ameongeza kuwa Tehran ilikuwa ikijaribu kuathiri uchaguzi wa katikati ya muhula ambao utaamua iwapo Chama chake cha Republican kitaendelea kudhibiti Bunge la Marekani.
Pia amewahi mara kadhaa kuweka muda maalumu wa kukamilika kwa vita hivyo.



