Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameshtakiwa kwa kujaribu kutengua uchaguzi wa 2020 katika jimbo la Georgia.

Yeye na wengine 18 wameshtakiwa kwa makosa ambayo ni pamoja na ulaghai katika hati ya mashtaka 41 iliyotolewa kwa jopo la majaji kaunti ya Fulton.

Shtaka hilo ni mara ya nne kwa Trump kufunguliwa mashtaka ya jinai mwaka huu.

Alikanusha tuhuma hizo katika kesi zote. Wakili wa Fulton Fani Willis alianzisha uchunguzi Februari 2021 kuhusu madai ya kuingilia uchaguzi dhidi ya Bw Trump na washirika wake.

Orodha ya washtakiwa walioshtakiwa Jumatatu usiku ni pamoja na wakili wa zamani wa Trump Rudy Giuliani, mkuu wa zamani wa Ikulu ya White House Mark Meadows, wakili wa zamani wa Ikulu ya Marekani John Eastman na afisa wa zamani wa idara ya sheria, Jeffrey Clark.

By Jamhuri