Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ameshuhudia kusainiwa kwa fedha kiasi cha Sh. Billion 1.6 zitakazotolewa na Serikali ya Ufaransa kusaidia wasanii katika sekta ya filamu, muziki wa Singeli, ubunifu wa mavazi na eneo la uandishi wa vitabu kidijiti hapa nchini.

Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema hayo Agosti 18, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuendeleza sekta za sanaa kupitia Mfuko wa Msaada wa Ujasiriamali wa Kitamaduni Afrika wa Ufaransa ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazonufaika na mfuko huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu azungumza na wadau wa Sanaa na kazi za ubunifu wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuendeleza sekta za Sanaa kupitia Mfuko wa Msaada wa Ujasiriamali wa Kitamaduni Afrika wa Ufaransa Agosti 18, 2023 jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui.

“Fedha hizi zitakwenda moja kwa moja kwa taasisi hizi kupitia Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa cha ‘Alliance Française’ ambapo jumla ya Sh. Billion 1.6 zimetolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya maeneo haya na zitakwenda kuuza muziki wetu wa Singeli nje ya Tanzania katika mradi wake wa ‘Singeli to the world’” Katibu Mkuu Bw. Yakubu.

Mradi huo wa Singeli ambao asili yake ni Tanzania unatarajiwa kuibia vipaji vya muziki huo katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Morogoro kwa vijana wa kike na wa kiume ili kukuza na kuendeleza muziki huo ndani na nje ya nchi pamoja na kuwasaidia wafanyabiashara wa kitamaduni wa nchini ili kuimarisha uwezo wao wa kitaaluma.

Katibu Mkuu Bw. Yakubu amemshukuru Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui kwa msaada wanaotoa kwa sekta hizo ambazo zinaubunifu mkubwa kwa vijana na zinahitaji uwezeshaji ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui (katikati) azungumza na wadau wa Sanaa na kazi za ubunifu wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuendeleza sekta za Sanaa kupitia Mfuko wa Msaada wa Ujasiriamali wa Kitamaduni Afrika wa Ufaransa Agosti 18, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui amesema nchi 16 za Afrika zitanufaika na Mfuko huo ikiwemo Tanzania kwa lengo la kukuza tasnia ya utamaduni na ubunifu ambazo ni kipaumbele kwa Ufaransa ambapo mwaka 2022 wakati wa ziara ya kikazi ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Sluhu Hasaan nchini humo walikuwa na mjadala na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu masuala ya Utamaduni baina ya nchi hizo mbili.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu azungumza na wadau wa Sanaa na kazi za ubunifu wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuendeleza sekta za Sanaa kupitia Mfuko wa Msaada wa Ujasiriamali wa Kitamaduni Afrika wa Ufaransa Agosti 18, 2023 jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui.
Meneja wa muziki wa Singeli na Mkurugenzi wa Kituo cha Kukuza na Kuendeleza  vijana wenye vipaji kutoka mtaani Bw. Masudi Kandoro azungumza na wadau wa Sanaa na kazi za ubunifu wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuendeleza sekta za Sanaa kupitia Mfuko wa Msaada wa Ujasiriamali wa Kitamaduni Afrika wa Ufaransa Agosti 18, 2023 jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui (wa pili kushoto).
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akiwa katika picha ya pamoja na  wadau wa Sanaa na kazi za ubunifu mara baada ya hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuendeleza sekta za Sanaa kupitia Mfuko wa Msaada wa Ujasiriamali wa Kitamaduni Afrika wa Ufaransa Agosti 18, 2023 jijini Dar es Salaam.