Na WAF – Bukoba,JamhuriMedia,Kagera

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewatembelea watumishi wa afya waliowekwa sehemu maalumu ya uangalizi baada ya kuwahudumia wagonjwa wa Marburg walioripotiwa katila Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera.

Ziara hiyo ameifanya leo akiambatana na Wawakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Zabron Yoti na Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bi. Shalini Bahuguna baada ya kutembelea katika Vijiji vya Kata ya Maluku na Kanyangele ambapo ugonjwa huo umeanzia

Waziri Ummy amewatia moyo watumishi hao kwakuwa Serikali ipo pamoja nao na lengo ni kuendelea kuwalinda wao na wanaowazunguka ikiwemo familia zao.

“Niwatie moyo ndugu zangu huu ugonjwa utaisha kwakuwa Serikali imedhamiria kuendelea kupambana ili kutokomeza kabisa na hali itarudi kama zamani.

Mwisho, Waziri Ummy amewataka watumishi hao wa Afya kuzingatia Kanuni na Taratibu za Udhibiti wa Maambukizi (Infection Prevention and Control) wakati wote wanapowahudumia wagonjwa.

By Jamhuri