na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar

Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete(JKCI) kwa kushirikiana na madaktari kutoka India wamefanikiwa kubadilisha valvu ya moyo bila kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa mara ya kwanza nchini .

Upasuaji huo ujulikanao kuwa wa tundu dogo ulichukua saa moja umefanywa kwa watu watatu ambao hali zao zinaendelea vizuri sasa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa JKC, Dk Richard Kisenge amesema awali wagonjwa wenye tatizo hilo walikuwa wanapelekwa nje ya nchi.

Dk Kisenge ameeleza kuwa upasuaji huo umefanywa na wataalamu wazawa kwa asilimia 90.

“Upasuaji huu unafanyika Ulaya na Asia na kwa Afrika wanaofanya ni Afrika Kusini, Misri, Tunisia na Morocco na hakuna hospitali ya Serikali  Afrika inayofanya aina hiyo ya upasuaji,”amesema.

Amesema upasuaji huo unagharimu kiasi cha Sh milioni 80 ndani ya nchi huku nje ya nchi ukiwa ni Sh milioni 150.

“Faida ya upasuaji huo ni kwamba inapunguza muda wa kukaa hospitali hii ni njia sahihi tunawafanyia bila kupasua kifua na hivi karibuni pia tumefanya upasuaji wa kuzibua mishipa ya miguu tulikuwa hatufanyi mwanzo.

Dk Kisenge amesema tayari nchi 20 za Afrika zimepeleka wagonjwa wao kutibiwa hivyo nafasi iliyopo sasa haitoshi na wagonjwa zaidi kutoka nje wataendelea kuletwa.

” Tuna uhitaji wa haraka wa kujenga hospitali, kuna wagonjwa wengi nilizungumza na Zaire wanataka kuleta wagonjwa hata Malawi pia wanatarajia kuleta wagonjwa hapa na taasisi inakwenda kuchangia pato la nchi kwani asilimia 97 ya matibabu ya moyo yanatibika hapa 

Please follow and like us:
Pin Share