Umoja wa Mataifa umeitenga Urusi siku ya Alhamisi, wakati wa kuadhimisha mwaka mmoja tangu Urusi ilipoivamia Ukraine huku ikitoa wito wa kuwepo kwa “amani na haki ya kudumu” na kuitaka tena Urusi kuondoa wanajeshi wake na kuacha mapigano.

Siku moja tu baada ya mwanadiplomasia mkuu wa China kuitembelea Urusi na kuahidi ushirikiano zaidi na Urusi, China haijapiga kura kwa mara ya nne dhidi ya hatua ya Urusi kuivamia Ukraine mnamo Februari 24 mwaka jana.

Azimio lilipitishwa siku ya Alhamisi kwa kura 141 za ndio na 32 hazikuhudhuria.

Nchi sita ziliungana na Urusi kupiga kura ya hapana – Belarus, Korea Kaskazini, Eritrea, Mali, Nicaragua na Syria.

“Azimio hili ni ishara kuu ya kuungwa mkono kimataifa kwa Ukraine,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alichapisha kwenye kurasa ya Twitter baada ya kura hizo.

Naibu Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Dmitry Polyanskiy alipuuzilia mbali hatua hiyo ya Umoja wa Mataifa kuwa “isiyo na maana,” akichapisha kwenye Twitter:

“Je, italeta amani? Hapana! Je, itawatia moyo wachochezi wa vita? Ndiyo! Hivyo hii ni kurefusha janga la Ukraine.”

Urusi ilikuwa imelitaja azimio hilo kuwa “lisilo na usawa na chuki dhidi ya Urusi” na kuzitaka nchi kupiga kura ya hapana ikiwa haziwezi kufanyiwa marekebisho.

Mshirika wa Urusi, Belarus alishindwa katika jaribio hilo la kubadilisha maandishi na marekebisho ikiwa ni pamoja na “kuzuia kuongezeka zaidi kwa mzozo kupitia kuwapa wahusika silaha.”

Mataifa ya Magharibi yameipatia Ukraine silaha za mabilioni ya dola tangu Urusi ilipovamia.

Marekani na NATO katika wiki iliyopita waliishutumu China kwa kufikiria kusambaza silaha kwa Urusi na kuionya China dhidi ya hatua hiyo

By Jamhuri