Kwa mara ya kwanza wanasayansi wamegundua pango la makazi mwezini.
Pango hilo lenye kina cha mita 100, linaweza kuwa mahali pazuri kwa wanadamu kujenga makazi ya kudumu.
“Ni moja tu kati ya mamia ya mapango yaliyofichwa katika ulimwengu wa chini ya ardhi, ambao haujagunduliwa”walisema watafiti.
Watafiti hao wameendelea kusema kuwa watu wengi wameshaonesha nia ya kuishi kwenye pango hilo lililoko mwezini, lakini watahitajika kujilinda dhidi ya mionzi, halijoto kali na hali ya hewa ya anga.
Mwanaanga wa kwanza kusafiri mwezini kutoka nchini Uingereza,Helen Sharman amesema ugunduzi wa pango hilo jipya ulionekana kama mahali pazuri pa kuishi kwa miaka 20 hadi 30.
“Hili pango lina kina kirefu lakini wanaanga wanaweza kuhitaji kujificha ndani na kutumia lifti kwa ajili ya kutoka” amesisitiza Sharman.
Chanzo: BBC