Na Mwandishi Wetu – ORPP, Morogoro
Wanasiasa waombwa kuwa mabalozi wazuri wa mahusiano baina ya Serikali na makundi mbalimbali ya kijamii katika kuimarisha mshikamano, amani, haki,upendo na utulivu katika kuendeleza umoja wa kitaifa na ustawi wa jamii.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Bibi. Zuhura Yunusi wakati akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa katika kikao kilichofanyika leo tarehe 20 Mei, 2026 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ruaha uliopo Nashera Hotel Mjini Morogoro.
“Lengo la kuja kwenu ni kuitambulisha rasmi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano pamoja na kutoa elimu kuhusu jukumu jipya la Idara ya Mahusiano pamoja na majukumu ya Idara husika.
Kwa Upande wake Msajili wa Vyama Siasa Jaji Mstaafu Francis Mutungi amesema kuwa ni wazi kwamba sote tunatambua umuhimu wa uhusiano na ushirikiano nakuongeza kuwa kunapokuwa na uhusiano kunazaliwa ushirikiano ambao unazaa majadiliano na hatimaye kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazotukabili.
Jaji Mutungi ameongeza kuwa viongozi wa vyama vya siasa ni wadau muhimu wa amani katika jamii kwa kuhakikisha wanahamasisha utulivu kutunza tunu ya amani iliyoasisiwa na waasisi wa taifa letu.
Naye Katibu Mkuu wa Cha cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Baraza la Vyama vya Siasa amesema kuwa panapokuwepo na mahusiano mazuri ndipo malengo yanafikiwa kwa ufanisi zaidi, kwa hiyo kunapokuwa na mahusiano mazuri katika Serikali na wadau wake tukiwemo viongozi wa vyama vya siasa
“ Na hiyo ni popote tu hata kwenye ndoa panapokuwa na mahusiano mazuri ndipo hata kwenye ndoa yale malengo ya nyinyi kuwa wana ndoa yanafikiwa kwa ufanisi zaidi mnapokuwa katika mahusiano mazuri” alisema Mwalimu.
Salum Mwalimu ameongeza kuwa kunapokuwa na mahusiano mazuri baina ya serikali na wadau wake ikiwemo vyama vya siasa maana yake ni kwamba kunakuwa na utekelezwaji wa mipango ya serikali masalani utekelezwaji wa mpango wa dira ya taifa ya 2050.
Mafunzo haya yamefanyika ikiwa ni maombi maalum ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) katika kutekeleza majukumu yake ya kuimarisha mahusiano baina ya Serikali na wadau wake ambapo kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa waliomba kukutnishwa na wajumbe hao na kuwapaitia elimu kuhusu majukumu ya Idara ya Mahusiano.




