Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akibadilishana hati ya mkataba na msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), mara baada ya kusaini mkataba huo. Mkataba huo ambao pia msanii Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley amesaini na kampuni hiyo, waasanii hao wameingia makubaliano kushiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania.

 

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akisaini mkataba na msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), mkataba huo ambaao pia Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley amesaaini na kampuni hiyo ili waasanii hao kushiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania.
 
SHIRIKA  la Mawasiliano Tanzania, TTCL leo limetiliana
saini na wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Zuena Mohamed maarufu
kama Shilole ‘Shishi Baby’ na Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley  watakaoshiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi
Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania.
 
Akizungumza na
Waandhishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri
Kindamba amesema Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasilino  Mhandisi Isaack
Kamwelwe Agosti 31 mwaka huu Mkoani Katavi.
Amesema lengo la
Kampeni hiyo ni kuwafikishia taarifa wananchi kuhusu TTCL mpya ambayo kwa sasa
imefanya mabadiliko makubwa katika biashara ya Huduma za Mawasiliano hapa
Nchini.
 
Asema Tamasha hilo
ambalo halitakuwa na kiingilio litakuwa la aina yake ambapo wasanii wamejipanga
kutoa burudani kabambe huku wananchi wakipata fursa ya kuelimishwa kuhusu
Shirika la TTCL, Huduma zake na majukumu yake ya msingi pamoja na  kujipatia Sim Kadi na kujisajili bure na
kuuziwa bidhaa mbalimbali za TTCL kwa bei nafuu.
 
“Hii ni kampeni ya Mkoa
kwa mkoa, ambayo pia itatumika kutatua changamoto na kero mbalimbali walizonazo
wateja wetu juu ya huduma na bidhaa zetu” alisema Kindamba
Kwa upande wake Zuena
Mohamedi kw aniaba ya msanii mwenzake amesema amejipanga kutoa burudani kabambe
itakayotoa hamasa kwa wananchi kupenda vya kwao na hivyo kurudi nyumbani kwa
kutumia Mtandao wa TTCL.
 
“Nawaomba Watanzania
wenzangu tuwe wazalendo tutumie bidhaa za nyumbani, mfano mimi nina line ya
TTCL ambayo intaneti yake ni ya kasi zaidi inaniwezesha kufanya kazi zangu kwa
urahisi  ikiwa ni pamoja na kuendesha
Akaunti zangu katika mitandao mbalimbali ya kijamii” alesema Shilole.
TTCL imedhamiria kuwa
Shirika kinara katika utoaji wa huduma za Mawasiliano Nchini, nafasi iliyokuwa
nayo hapo awali. Kupitia maboresho makubwa inayoyafanya, TTCL imeweza kutoa
gawo la Tsh Bilioni 1.5 mwaka huu wa fedha na kuahidi kuongeza kiasi cha gawio
katika miaka inayofuata sambamba na kuongeza uwekezaji katika teknolojia za
kisasa, ubora wa huduma na ushiriki wa TTCL katika kutoa ajira kwa Watanzania
na kusaidia shughuli za kijamii.
 
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akibadilishana hati ya mkataba na msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), mara baada ya kusaini mkataba huo. Mkataba huo ambao pia msanii Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley amesaini na kampuni hiyo, waasanii hao wameingia makubaliano kushiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania.
 
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla hiyo ya kusainishana mkataba.

 

Msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ya kusainishana mkataba.

By Jamhuri