Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema ulinzi na
usalama wa Tanzania ni wajibu wa kila mwananchi, akisisitiza kuwa kila
Mtanzania anatakiwa kushiriki katika kulinda amani, umoja wa kitaifa
na mali za umma kwa kuzingatia Katiba na sheria za nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Julai 2,
2026, Katambi amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuzuia
uhalifu kabla haujatokea kwa kubaini mianya, tabia na viashiria
vinavyoweza kusababisha vitendo vya uhalifu.
Aliwataka wananchi kuendelea kuheshimu sheria za nchi na kutumia
taratibu za kisheria pale wanapodhani haki zao zimekiukwa, badala ya
kujichukulia mamlaka
Amesema hivi karibuni kumekuwa na upotoshaji kuhusu haki ya
kukusanyika na kushirikiana na wengine, akieleza kuwa ingawa ni haki
ya msingi inayotambuliwa na Katiba, utekelezaji wake unapaswa
kufanyika kwa kuzingatia masharti ya kikatiba na kisheria.
‘’Nimelazimika kutoa ufafanuzi wa msini kuhusu maswali ,hoja mjadala
na upotoshaji wa kujua ama kutokujua unao endelea katika jamii ya
watanznia, kuhusu ulinzi na usalama wa raia na mali zao pamoja na haki
za watu,mali za kila mtu ,utajiri au maliasili za nchi yetu na wajibu
wa kila mwananchi
Ifahamike na kueleweka kuwa wizara ya mambo ya ndani ya nchi ndiyo,
yenye dhamana ya usalama ndani ya nchi kwa kuhakikisha muda wote nchi
inakuwa chini yake
Hivyo wizara ina wajibika kutekeleza jukumu hilo kwa wivu mkubwa wa
kubaini na kutambua viashiria ,ishara ,fursa,mianya ,tabia mipango au
maandalizi ya uhalifu kabla haujatokea na kuchukua hatua mapema ili
kuhakikisha visababishi husika visihitimu na kusababisha
uhalifu’’amesema
Katambi amesema ni vyema umma ukatambua kuwa hoja ya waziri kuwa na
mamlaka au kutokuwa na mamlaka na uvunjaji wa katiba ya Jamhuri ya
Muunganowa Tanzania ,1977 sitoweza kujadili na kutolea ufafanuzi hadi
hapo wanaodai upo uvunjifu wa katiba watakapo kwenda kufungua shauri
mahakamani
‘’Nasema haya kwasababu hakuna mtu au taasisi ambayo ina mamlaka ya
kikatiba ya kutoa hukumu isipokuwa mahakama pekee kwa mujibu wa ibara
ya 107A(1)ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’amesema
Aidha amesema hakuna ubishi kwamba uhuru wa mtu kushirikiana na
wengine ni moja ya haki za msingi zilizo ainishwa katika katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,1977
Isipokuwa uhuru huo wa kushirikiana na wengine na kufanya mkutano ya
hadhara na kukusanyika si haki kamili ,haki hii inaweza tu kuwa kamili
ikiwa inatekelezwa kwa kufuata masharti yaliyowekwa kwa mujibu sheria
yeyote iliyotungwa na bunge hasa inayolinda maslahi ya umma usalama
Amani afya ya jamii na uhuru na haki za wengine
Amesema ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ndiyo
msingi mkuu wa uhuru wa kushirikiana ,ambayo imeweka na kutambua haki
ya kila mtu kwa mujibu wa sheria kukutana kukusanyika kwa amani
kuandamana na kushiriki mikutanoi ya umma
Wajibu wa kulinda taifa umeainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, akibainisha kuwa kila raia ana
jukumu la kulinda uhuru, mamlaka, ardhi, umoja wa taifa pamoja na
kuheshimu mali za umma na za watu binafsi.
Amesema kifungu cha 42 cha sheria ya jeshi la polisi na huduma saidizi
,sura ya 322 kimeweka masharti mbalimbali kuhusu usimamizi na uratibu
wa mikusanyiko na kinawapa Jeshi la Polisi lina mamlaka ya kuelekeza
namna mikusanyiko na maandamano yatakavyo endeshwa ikiwa ni pamoja na
njia na muda kwa ajili ya kudumisha utulivu na usalam kwa kila mtui
mali na umma kwa ujumla.
Katambi amedai kwa kuzingatia maelekezo ambayo ni msingi wa kikatiba
na sheria msimamo wa kisheria nchini , kufanya mikutano ya hadhara ni
haki ya kikatiba ,lakini utekelezaji wake unaweza kuwekwa chini ya
masharti ya sheria yanayolenga kulinda usalam ,utulivu wa ummana haki
za wengine



