Na Magrethy Katengu, JamuhuriMedia, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na maofisa wa mifumo ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 30 kwa tuhuma za kugushi nyaraka mbalimbali zinazohusiana na mfuko wa mafao ya NSSF kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia ya uhalifu.

Akizungumza leo Aprili 9,2024 Kamanda wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao ni pamoja na mwalimu wa Shule ya Msingi Maximilian ya Segerea Deocres Kagwa umri 35 ambaye alikuwa na Barbanas Bonivanture na wenzao 11wa Kampuni binafsi ya Ulinzi G4S ambao kwa nyakati tofauti tofauti waliwasilisha nyaraka za uongo za hati ikiwemo za kufukuzwa kazi, matibabu,wakiwa na lengo za kujipatia fedha za mafao kutoka katika mfuko huo.

Sambamba na hayo lamanda amewataja watu wengine waliokamatwa ni Mtumishi wa Benki ya Stanibic Mkazi wa Upanga Prygod Rwekiza (37), Michaeli Mpogolo na Sabato Thomasi umri (38) nao wanatuhumiwa kugushi nyaraka za taarifa za hospitali wakilenga mafao ya matibabu pia nyaraka za watu ambao walishariki ambao walifanya kazi kazi ya uchimbaji madini Geita.

“Kupatikana kwa watuhumiwa hawa ni kushukiwa lampuni moja kuwa na nyaraka za watu wengi walioacha kazi mara moja na wengine kufukuzwa hivyo Wataalamu walifuatilia kwa kina na kugundua kuwa kumbe nyaraka nyingi zilikuwa za kugushiwa hivyo wakashirikisha Jeshi la Polisi kufuatilia kwa karibu na kuwakamata watuhumiwa hao hivi karibuni watafikishwa mahakamani” amesema Kamanda.

By Jamhuri