Na Mussa Augustine.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano kubwa la aKitaifa la kuwajengea uelewa viongozi wa dini mbalimbali kuhusu athari zitokananzo na sauti zilizozidi Viwango katika Nyumba za ibada.

Hayo yamesemwa Juni 8 ,2023 na Mwenyekiti Taifa wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania(JMAT) Shekh Alhad Mussa Salum wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam ambapo amesema kongamano hilo litafanyika jumatatu ya Junib12 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere( JNICC).

Aidha Shekh Alhad Mussa amesema kwamba Kongamano hilo litawahusisha viogozi wa dini pamoja na viongozi wa kimila ikiwa lengo ni kupatiwa elimu kutoka kwa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC ili wajue ni kiwango gani cha sauti wanachopaswa kukitumia katika nyumba zao za ibada.

“Nawaomba Viongozi wote wa dini Wahudhurie kupata elimu hiyo Kutoka NEMC,mada zipatazo tisa zitajadiliwa ikiwemo mada kuhusu Utiifu kwa Mamlaka kwa Mujibu wa Biblia pamoja na Utiifu wa Mamlaka kwa Mujibu wa Qur’an na Sunna” Amesema Shekhe Alhaji Mussa.

Nakuongeza kuwa ,”Mada zingne zitakazojadiliwa ni Uchungaji wa Haki katika Ibada na Haki za wengine kwa Mujibu wa Qur’an na Sunna,pia Uchungaji wa Haki katika Ibada na Haki za wengine kwa mujibu wa Biblia ,Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004 na kanuni zake,Athari zitokanazo na Sauti zilizozidi kiwango” amesema Shekhe Alhaj Mussa

Aidha amendelea kusema kwamba Mada za Usimamizi wa Mipango Miji,Uelewa kuhusu Sheria na Kanuni za Usajili wa asasi za kiraia,pamoja na Majukumu na Wajibu wa RITA kwa Taasisi za Kidini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazungira (NEMC) Dkt Stanley Gwamaka amesema kwamba Kongamano hilo linatokana na agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye aliitaka NEMC ikutane na Viongozi wa Dini na Kimila ili kuwapa elimu kuhusu kiwango cha Sauti inayotakiwa kwenye nyumba za Ibada.

” Moja ya jukumu letu sisi NEMC ni kutoa elimu ya utunzaji wa Mazingira kwa jamii,hivyo kuna kiwango cha sauti kilichopo kisheria ambacho lazima kifuatwe ili kuweka mazingira safi na salama kwa wananchi waweze kushiriki kwenye shughuli zao za kiuchumi” amesema Dkt Gwamaka

Nakuongeza kuwa ” Hata kama una furaha au huzuni kiasi gani bado kuna kiwango cha sauti kilichopo kisheria ambacho unapaswa kutumia,hutakiwi kuweka sauti kubwa ambayo inasababisha athari kubwa kwa wengine.