Timu ya Taifa ya Zanzibar , Zanzibar heroes imezidi kuonyesha maajabu yake kwenye michuano ya CECAFA, baada ya leo kuwatoa mabingwa watetezi Ugnada kufuatia kipigo cha 2-1 na kutinga hatua ya fainal ambapo watakutana na timu ya Taifa ya Kenya.

Timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars imetinga hatua ya Fainali ya Michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup baada ya kuifunga Burundi kwa 1-0, bao lililofungwa katika dakika ya 97 ndani ya Dakika 120 za nyongeza baada kushindwa kufungana katika dkk 90 za mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa katika dimba la Moi, mjini Kisumu jana.

Zanzibar Heroes itakutana na wenyeji Kenya Harambee Stars siku ya Jumapili katika mchezo wa fainali. Katika mchezo wa makundu timu hizi zilipokutana zilitoka sare ya kutofungana

Please follow and like us:
Pin Share