Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Bunge, Chacha Nyakega akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Baraza hilo limemaliza kipindi chake cha miaka mitatu
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu akitoa hotuba ya kuvunja Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Baraza hilo limemaliza kipindi chake cha miaka mitatu.
Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi akitoa hotuba ya kumkaribisha Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Spika Mhe. Mussa Zungu kwa ajili ya kulivunja Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge baada ya Baraza hilo kumaliza kipindi chake cha miaka mitatu. Kikao hicho cha Baraza kimefanyika katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.