Habari za Kimataifa

AJALI: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Apata Ajali ya Gari

AJALI: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Juma Kilimba amepata ajali ya gari lake kupinduka leo akiwa na familia yake, mke wake na watoto wawili wamepewa rufaa. Yeye bado na watoto wawili bado wako hospital ya Wilaya Kiomboi ambapo mtoto mmoja hawezi kusafirishwa hali yake sio nzuri, tumuombee  

Read More »

Catalonia Yashinda Uchaguzi ya Kutaka Kujitoa na Uhispania

Vyama vinavyounga mkono jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania vimeshinda uchaguzi wa jimbo la Catalonia. Ikiwa kura zote zinakaribia kukamillika kuhesabiwa Katika rekodi ya wapiga idadi ya wapiga kura ambao wamejitokeza vyama hivyo vinaonekana kushinda jambo kimepunguza kidogo idadi ya viti bungeni. Matokeo hayo kwa vyovyote ni habari mbaya kwa waziri mkuu wa Hispania,Mariano Rajoy ambaye aliingilia kati jimbo hilo ...

Read More »

Rais wa Ujerumani Ahimiza Ujenzi Taasisi Imara

Rais wa Ujerumani, Frank- Walter Steinmeir, amehitimisha ziara yake katika bara la Afrika kwa kuhimiza masuala ya demokrasia na maendeleo ya kiuchumi.  Katika ziara yake hiyo, Rais Steinmeir  amehimiza uimarishwaji vita dhidi ya ufisadi  na  mapambano imara juu ya  uhamiaji unaoendelea kuwa tishio kwa maisha ya binadamu hasa katika kipindi hiki. “Mataifa yote yanapaswa kuungana ili kukabiliana na janga hili linaloendelea ...

Read More »

Marekani Kufufua Mazungumzo Kati ya Israel na Palestina

Ikulu ya Marekani inatarajia kuanzisha upya juhudi za kufikiwa  kwa makubaliano ya amani kati ya Israel na Palestina, licha ya uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa Mji Mkuu wa Israel. Mpango huo wa Marekani unatarajiwa kuja baada ya awali kuliudhi taifa la  Palestina, mataifa ya Kiislamu na jumuiya ya kimataifa. Maafisa utawala wa Marekani wamesema juhudi hizo huenda ...

Read More »

UN Yakutana Kumjadili Trump

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeombwa kuitisha mkutano wa dharura  kujadili hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump  kuuhamisha Ubalozi wa Marekani kutoka Telaviv hadi Jerusalem. Maamuzi hayo yalisababisha maandamano makubwa yaliyosababisha watu 17 kujeruhiwa kwa risasi na jeshi la Israel wakati Wapalestina walipoandamana katika Ukingo wa Magharibi na ukanda wa Gaza. Lengo kuu la maandamano hayo ilikuwa ...

Read More »

Wanawake 24 Sudan Hatarini Kucharazwa Viboko 40 Kila Mmoja

Wanawake 24 wa Sudan wameshtakiwa kwa kujivunjia heshima, baada ya kuonekana wamevaa suruali katika karamu moja mjini Khartoum. Karamu hiyo ilivamiwa na polisi wa nidhamu siku ya Jumatano. Suruali zinachukuliwa na wakuu kuwa vazi la utovu wa adabu, na adhabu yake ni mijeledi 40 pamoja na faini. Wanaharakati wanasema maelfu ya wanawake wanakamatwa kila mwaka, na kuichapwa mijeledi. Wanasema sheria ...

Read More »

Polisi wa Israel Yawajeruhi Wapalestina Zaidi Ya 30 Ukanda wa Gaza

Vurugu zimeendelea huko ukanda wa gaza na ukingo wa magharibi ambapo zaidi ya wapalestina thelathini wamejeruhiwa katika makabiliano na polisi wa Israel Hii ni kufuatia Rais Donald Trump kutangaza kuutambua mji wa Yerusalemu kuwa mji mkuu wa Israel. Wakati huo huo Marekani imeionya Palestina dhidi ya maamuzi yake kutotaka kukutana na makamu wa rais marekani ,Mike Pence katika kikao ambacho ...

Read More »

Mahakama ya Liberia Yaruhusu Uchaguzi Kurudiwa Duru ya Pili

Mahakama kuu ya Liberia imesema kuwa ushahidi wa vitendo visivyokubalika katika uchaguzi wa Rais duru ya kwanza mwezi Oktoba hautoshi kuufanya uchaguzi kurudiwa. Hii inamaanisha kuwa mzunguko wa mwisho wa uchaguzi kati ya wagombea wawili waliokuwa wakiongoza yaani George Weah na Makamu wa Rais Joseph Boakai unaruhusiwa kuendelea. Sasa inasubiriwa tume ya uchaguzi kuweka na kuitangaza siku ya kupiga kura. ...

Read More »

Palestine Yagoma Kumkaribisha Makamu wa Rais wa Marekani

Marekani imeionya Palestina dhidi ya maamuzi yake kutotaka kukutana na makamu wa rais Marekani ,Mike Pence katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika mapema mwezi huu ili kujadili uamuzi wa rais Trump wa kuhamishia Yerusaleam kuwa mji mkuu wa Israel. Ikulu ya Marekani imesema, uamuzi huo uliofikiwa na Palestina utakuwa hauna maana kwa kuwa hawataweza kupata suhulu ya mgogoro huo. Makamu wa ...

Read More »

Marekani Yamnyoshea Kidole Odinga Mpango Wake wa Kutaka Kuapishwa

Marekani imemtaka kiongozi wa upinzani nchini kenya Raila Odinga kuacha mpango wake wa kuapishwa kama raisi wan nchi hiyo wiki ijayo. Odinga aliwasilisha Malalamiko juu ya mapungufu katika uchaguzi mkuu uliopita na kusababisha uchaguzi wa marudio ambapo Uhuru Kenyata alishinda kwa kura nyingi. Msaidizi wa katibu wa masuala ya Afrika Marekani , Donald Yamamoto ambae ametembelea nchini kenya. Ametaka majadiliano ...

Read More »

Vladimir Putin Atangaza Nia ya kuwania tena urais 2018

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kuwa atawania kiti cha urais kwa mara nyingine tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2018. Alitangaza hayo alipokuwa akiwahutubia wafanyikazi huko Nizhny Nov-gorod. Rais Putin ambaye ana umri wa miaka 65 alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Urusi mwaka 2000. Baada ya kuhudumu kwa mihula miwili alichaguliwa kama Waziri mkuu ...

Read More »

Rais Trump Sasa Aitambua Yerusalem ni Mji Mkuu wa Israel

Akiongea katika Ikulu ya Marekani, Rais Trump ameutambua mji wa Yerusalem kama mji mkuu wa Israel, maamuzi ya kihistoria yanayopindua sera za miaka mingi za Marekani. Rais Donald Trump ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka katika eneo la sasa la Tel Aviv kwenda Yerusalem. Amesema kuwa uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za kuleta amani katika ...

Read More »

Marekani Yaionyeshea Ubabe wa Kivita Korea Kaskazini

Jeshi la Marekani limerusha ndege yake aina ya B-1B bomber katika anga ya Korea Kusini kama sehemu ya mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua inayoonekana kama onyo kwa Korea Kaskazini. Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa marefu ambalo linaloweza kushambulia nchini Marekani. Marekani awali imerusha ndege hizo ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons