page za ndani

Mkurugenzi UCC ahusishwa kashfa nzito

Na Alex Kazenga Dar es Salaam Wafanyakazi zaidi ya 30 wa Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta (UCC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamo hatarini kupoteza kazi baada ya kituo hicho na matawi yake yote nchini kutakiwa kufungwa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni mbinu zinazoratibiwa na menejimenti kukiua kituo hicho. Anayetuhumiwa kufanya mbinu hizo ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo ...

Read More »

Korosho bado ni ‘umiza kichwa’! (1)

Nilifurahi mno Jumatano ya Septemba 5, mwaka huu nipoona katika runinga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gilasius Byakanwa, akiwa katika Kiwanda cha Korosho Tandahimba akitoa uamuzi wa serikali (kwa barua rasmi) kwa mwekezaji wa kiwanda kile kununua korosho kwa kufuata maelekezo ya serikali kupitia mnada wa stakabadhi ghalani. Na kwamba amalizapo kubangua afuate sheria za ununuzi wa korosho kama ilivyoelekezwa ...

Read More »

Jela si mchezo

DAR ES SALAAM NA WAANDISHI WETU Kishindo kikubwa kinatarajiwa kuanza kusikika wiki hii baada ya mabadiliko ya uongozi katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Mtikisiko huo, pamoja na mambo mengine, utawahusisha baadhi ya vigogo wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi. Tayari kuna orodha ndefu ya majina ya watu wanaokusudiwa kufikishwa kwenye ‘Mahakama ya Mafisadi’ kujibu tuhuma zinazowakabili. Kwenye orodha ...

Read More »

Makonda azua balaa bandarini

Na Mwandishi Wetu Makontena aliyoingiza nchini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, yameleta ‘shida sana’ bandarini na sasa mfumo wa kutoa na kuingiza makontena kwenda kwenye ICD utabadilishwa, JAMHURI limebaini. “Kwa kweli hapa tulikuwa tunaangalia bill of lading na taarifa za mzigo (cargo manifest). Lakini pia kule TICTS walikuwa bado wanaweza kutoa makontena kwenda kwenye ICDs (Bandari ...

Read More »

Bemba abeza uchaguzi DRC

Aliyekuwa mgombea urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jean- Pierre Bemba, ameubeza uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Desemba 23, mwaka huu kwa kuufananisha na maigizo yaliyopangwa kutimiza matakwa ya wachache. Akizungumza na wanahabari mara baada ya jina lake kuwa miongoni mwa wagombea sita walioenguliwa na Mahakama Kuu nchini humo, amesema wananchi wa Congo hawatakuwa tayari kuchaguliwa kiongozi na kikundi ...

Read More »

Macron na Markel wajadili uhamiaji

  Marseille, Ufaransa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, wamekutana mjini Marseille, Ufaransa kujadiliana kuhusu uhamiaji haramu kuelekea mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya Septemba 20, mwaka huu. Akimkaribisha Merkel katika kasri ya Pharo iliyoko katika mji wa Marseille, Macron amesema watajadili changamoto zinazohusu uhamiaji, kujitoa kwa nchi ya Uingereza katika Jumuiya ya Ulaya ...

Read More »

Rais Magufuli, meli umefuta kero

Wiki iliyopita Rais John Magufuli amefanya ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Moja ya ziara zilizotugusa ni ziara aliyoifanya mkoani Mwanza. Akiwa Mwanza amezindua ujenzi wa meli kubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria 1,200, mizigo tani 400 na magari 20. Ujenzi wa meli hii mpya utakwenda sambamba na ukarabati wa meli za MV Victoria na MV Butiama. Pia rais ...

Read More »

Ndugu Rais, wewe si mwanasiasa mzuri

Ndugu Rais, hakuna siku uliuchoma moyo wangu kama siku ile uliyo wazi, tena kwa umakini mkubwa huku ukionyesha waziwazi kuwa makali ya hisia katika kifua chako. Ukafika mahali ukashindwa kujizuia Naona uchungu ulikuzidi. Ilipokuja afueni, ukatulia kidogo. Na kama lilikujia, kwa unyenyekevu mkubwa ukasema: “Nadhani mimi si mwanasiasi Kikafuata kimya kingi. Baba, maneno yako yaliuumiza sana moyo wangu Kwa kauli ...

Read More »

Parking Airport ni hatari

Mpita Njia (MN) amepata fursa ya kwenda Uwanja wa Ndege wa zamani wa Dar es Salaam (Terminal I). Akiwa hapo uwanja wa ndege langoni alikuta teknolojia ya kisasa kabisa, ambapo gari kuingia unabonyeza mashine, bonyeee, inatema kadi ya kulipia gharama za kuingia uwanjani hapo. MN kwake ni kawaida kuingia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Dar es Salaam ...

Read More »

Wingu jeusi’ linamnyemelea Koffi Olomide (2)

  …Kutokana na tukio hilo Serikali ya Kenya ilimuamuru mwanamuziki huyo mwenye sauti nzito kuondoka mara moja nchini humo kutokana na kutokubaliana na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake. Onyesho lililokuwa limepangwa kufanyika lilifutwa, wapenzi na mashabiki wake wakibaki wakisubiri kwa hamu. Kama hiyo haitoshi, mwaka 2012, Olomide alipatikana na hatia ya kumshambulia na kumjeruhi msimamizi wake wa karibu, Diego Lubaki, ...

Read More »

Maana ya hisa na aina zake kisheria

NA BASHIR YAKUB 1. Nini maana ya hisa? Hisa ni masilahi ya kila mwanachama aliyonayo katika kampuni fulani. Yaani wewe kama ni mwanahisa katika kampuni fulani, basi yale masilahi yako au kiwango chako cha uwekezaji ulichowekeza katika ile kampuni ndizo hisa zako. Kama mko watu kumi katika kampuni, basi kila mtu ana masilahi au kiwango kadhaa cha uwekezaji, ambapo ukikusanya ...

Read More »

Ukombozi wa fikra kwa Watanzania (3)

Na William Bhoke Kwa uhalisia wake, bado Watanzania hatujajitambua, Watanzania tumekuwa kama mbuzi wa kiangazi. Mbuzi wa kiangazi wanazunguka kutwa nzima pasipo kuelewa wanaelekea wapi. Imepita takriban miaka 54 tangu taifa hili kupata uhuru, lakini cha ajabu ni kwamba bado taifa linachechemea katika huduma za kimaendeleo. Nchi yetu inahitaji mabadiliko kama vile mtu aliyekabwa koo anavyohitaji hewa ya oksijeni. Huyu ...

Read More »

LINI WATATHAMINIKA?

LINI WATATHAMINIKA 1: Japo wao ndo walezi, thamani yao ni ndogo, Hufanyishwa ngumu kazi, kuzidi punda mdogo, Wengi hutokwa machozi, ya kulemewa mizigo, Mama zetu vijijini, lini watathaminika? 2: Masaa kumi na mbili, mama anachapa kazi, Lile jua lote kali, lamuishia mzazi, Uko wapi uhalali, baba kutofanya kazi? Mama huzalisha mali, lakini hanufaiki. 3: Kweli wanasulubika, kwa hizi adhabu kali, ...

Read More »

CHAKUA walilia ruzuku, kuwapigania abiria

NA AGUSTINO CLEMENT, TUDARCO DAR ES SALAAM Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua) kimesema kimekuwa na wakati mgumu wa kutimiza majukumu yake ya kutetea haki za abiria kutokana na kukosa ruzuku kutoka serikalini. Chakua imekuwa ikiahidiwa na serikali kupata ruzuku hiyo kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kwa muda mrefu lakini utekelezaji huo umekuwa ...

Read More »

Sheria mpya ya kulinda barabara kuanza Januari

NA MICHAEL SARUNGI, DAR ES SALAAM Serikali imetangaza kuanza kutumika kwa sheria mpya ya udhibiti wa uzito wa magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa Vehicle Load Control Act, 2016) kuanzia Januari mwakani ili kukabiliana na uharibifu wa barabara pamoja na majanga mengine. Akizungumza na wadau wa sekta ya ujenzi katika mkutano uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni, Katibu Mkuu ...

Read More »

Zimamoto na Uokoaji wasaidiwe kukabili changamoto

Na Zulfa Mfinanga, Dodoma Licha ya kuwepo kwa Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchin haina mfumo wa dharura wa uokoaji katika ajali za barabarani. Sheria ya Zimamoto na Uokoaji Cap 427 ya mwaka 2008, Kifungu c cha (1) cha sheria hiyo kimeeleza majukumu ya jumla ya jeshi hilo kupunguza idadi ya vifo, kupunguza na kuzuia madhara kwa binada ...

Read More »

MAFANIKIO YOYOTE YANA SABABU (37)

Na Padri Dk. Faustine Kamugisha Moyo ni sababu ya mafanikio. Unapoweka moyo wako wote katika lile unalolifanya utafanikiwa. “Fanya kazi kwa moyo wako wote, na utafanikiwa – kuna ushindani mdogo, ” alisema Elbert Hubbard. Kuna methali ya Tanzania isemayo: “Moyo uutulize sehemu moja kama mbwa anapopikiwa panya.” Kinachobainishwa hapa ni kuwa na moyo usiogawanyika. Mtaka yote kwa pupa hukosa yote. ...

Read More »

Bandari: Hatua za kuagiza mzigo nje ni hizi

Na Mwandishi Maalumu Kutokana na maombi ya wasomaji wa makala za Bandari ku JAMHURI, ambao wameomba turudie kuchapisha baadhi ya kuwathamini wasomaji na wadau wetu tumekubali kurudia makala h Moja ya makala ambazo wasomaji wetu waliomba turudie ni ya ambazo mwagizaji wa mzigo kupitia bandari zetu anapaswa kuagiza na kuupata mzigo wake kwa njia rahisi. Hatua hizo ni k haujafika ...

Read More »

Ni neema ya Mungu, nilikiona kifo – Kigwangalla

*Asimulia tukio zima la ajali waliyoipata, aelezea afya yake *Awashukuru wananchi kwa kumwombea *Alitangaza wosia, watu anaowadai na wanaomdai Nianze kwa msemo maarufu wa lugha ya Kiswahili usemao: “Kama haujui kufa, tazama kaburi.” Anayeweza kuthibitisha maneno haya ni yule aliyenusurika katika matukio mabaya ambayo yangeweza kusababisha kifo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla, ambaye amenusurika kifo katika ajali ...

Read More »

Makala: Jinsi Waafrika Walivyonyimwa Bia

Sehemu ya tatu, mwandishi wa makala hii aliishia kwenye maelezo ya namna Waafrika walivyozuiwa kunywa bia katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo iliibua mgogoro mkubwa. Sehemu hii ya nne na ya mwisho, mwandishi anaeleza umuhimu wa Waafrika kujiamulia mambo yao wenyewe badala ya kutegemea Marekani na Ulaya. Endelea… Wazungu wote kwa ujumla wao hawakutuona sisi ...

Read More »

Diwani kituko, anawaliza wananchi

Na Helena Magabe, Tarime Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa dhahabu wa Kebaga uliopo Kata ya Kenyamanyori, Tarime, Mkoa wa Mara, wamemlalamikia diwani wa kata hiyo kwa kuwanyanyasa vijana pamoja na wachimbaji wadogo. Diwani huyo aitwaye, Ganga Ganga, anatuhumiwa kuwakamata watu hao kwa kutumia ushawishi wa Jeshi la Polisi, kuwatesa, pamoja na kuwazuia kuchimba dhahabu kwa sababu zisizo za msingi. ...

Read More »

Asante rais kwa kuusema ukweli

NA ANGELA KIWIA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, kwa kuchapa kazi kimyakimya na kuleta maendeleo makubwa katika mkoa wake. Rais Magufuli amebainisha kwamba Mtaka ndiye kinara katika wateule wake wa ngazi ya mikoa nchini. Amesema kuwa Mtaka ndiye mkuu wa mkoa anayeongoza kwa kufanya kazi vizuri kuliko ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons