Siasa

Aliyekamatwa na Mabilioni Airtport Aachiwa Huru

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru na kumrudishia fedha zake, Winfred Busige (33), raia wa Uganda aliyekamatwa akisafirisha fedha kiasi cha TZS bilioni 2, katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JKNIA), baada ya kulipa faini ya TZS milioni 100.

Read More »

Joshua Nassari Apandishwa Kortini kwa Kumpiga Diwani

Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Joshua Nassari leo Februari 6, 2018 amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kusomewa shitaka linalomkabili. Katika kesi hiyo, Nassari anakabiliwa na tuhuma za kumshambulia na kumsababishia maumivu kwa aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Makiba mwaka 2014, Neema Ngudu. Aidha, Nassari ameachiwa kwa dhamna na kesi hiyo kuahirishwa hadi Machi 6, itakapotajwa ...

Read More »

Mahakama Yaagiza Nabii Titto Apime Upya Akili

MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imeagiza mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma Tito Machibya, maarufu kama ‘Nabii Tito’ (45) kupimwa akili upya katika Taasisi ya Afya ya Akili ya Mirembe Isanga mkoani Dodoma ili kuriridhisha kama ana matatizo ya akili. Licha ya kuagizwa mtuhumiwa huyo kufanyiwa vipimo upya, mahakama pia imetaka kuwasilishwa kwa vielelezo kama kweli ana tatizo hilo kama ...

Read More »

TUNDU LISSU AZUNGUMZA NA MAOFISA WA MAKAO MAKUU WA UMOJA WA ULAYA (EU)

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema jana alitembeleawa na Maofisa watatu kutoka Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa ajili ya kumjulia hali na kuzungumza naye juu ya masuala mbali mbali yanayoihusu Tanzania. Tundu Lissu amesema kuwa Ujumbe wa EU umeongozwa na Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki ...

Read More »

WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA UTAFITI WA MAPATO,MATUMIZI KWA KILA KAYA GEITA

Mkuu wa mkoa Geita ,mhandisi Robert Luhumbi kushoto akiwa na Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafisi Tanzania Bara wa mwaka 2017/18.  Katibu tawala wa Mkoa wa Geita,Celestine Gesimba akimkaribisha mkuu wa mkoa kuzungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti wa mapato ...

Read More »

MANGE KIMAMBI AMCHEFUA SHEKHE MKUU WA DAR ES SALAAM, SASA KUKIONA CHA MOTO

SHEHE  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa amemuonya mwanaharakati maarufu, Mange Kimambi kwa madai kuwa amemporomoshea matusi mazito baada ya kumuona mtandaoni amepiga picha na mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulya. Shehe Alhadi ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa picha ...

Read More »

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI MAZIKO YA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU

Rais dkt. Magufuli leo ameshiriki maziko ya mwanasiasa mkongwe marehemu mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika makaburi ya Kinondoni jijini dar es salaam Mazishi hayo pia yaliuzuriwa na Marais wastafufu, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete, pamoja na Viongozi wengine wa Serikali na wa vyama vya siasa akiwepo Waziri mstaafu Lowassa na Mwenyekiti wa CHADEMA  Mh. Mbowe.  

Read More »

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU ALIYEPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA BILA KIBALI

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachiwa huru mfanyabiashara Abdullah Hauga (73) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa kupeperusha bendera ya Tanzania bila kibali. Hatua hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Nolle Prosequi kuwasilisha chini ya kifungu cha sheria namba 91(1) cha mwenenendo wa makosa ya jinai kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya Hauga. Kabla ...

Read More »

MSIBA WA KINGUNGE WAWAKUTANISHA LOWASSA NA KIKWETE

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa Waziri Mkuu wake kabla ya kujiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa wameungana na mamia ya waombolezaji na viongozi wengine wa nchi katika kuuaga mwili wa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngiombale Mwiru leo jijini Dar es Salaam. Mbali na Mama Samia, Lowassa na Kikwete, viongozi wengine wengine waliohudhuria ni ...

Read More »

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aapishwa Rasmi Bungeni

NAIBU Spika wa Bunge, Dkt.  Tulia Ackson amemwapisha Mmwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dkt. Adelardus Kilangi bungeni na kumkabidhia vitendea kazi kabla ya kuanza kwa Kikao cha Tano cha Mkutano wa 11 wa Bunge, Mjini Dodoma, leo Feb 5, 2018. Dkt. Kilangi ambaye amekula kiapo cha uaminifu, aliteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Mgufuli,  Februari Mosi, 2018 na Paul Ngwembe aliteuliwa ...

Read More »

MGOMBEA UDIWANI WA CHADEMA APOTEA KIMIUJIZA, MKOANI KAGERA

Kampeni za ubunge na udiwani zikiendelea, mgombea udiwani (Chadema) Kata ya Buhangaza wilayani Muleba amepotea katika mazingira ya kutatanisha. Imeelezwa alipotea februari 2, 2018 alipokuwa akitokea Bukoba Mjini kwenda nyumbani kwake Kijiji cha Buhangaza ikidaiwa ametekwa. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Isack Msangi amethibitisha kupokea taarifa za kupotea kwa mgombea huyo. Amesema kuwa hawana madai kuwa ametekwa bali ...

Read More »

CHADEMA YATANGAZA KUSITISHA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA WABUNGE

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza kusitishwa kwa kampeni zauchaguzi wa Wabunge wa  chama hicho zinazoendelea, ili kushiriki maziko ya Mzee Kingunge Ngombale Mwiru. Mzee Kingunge alifariki juzi kwenye Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa majeraha ya kung’atwa na mbwa wake nyumbani kwake. Mzee Kingunge anazikwa leo Februari 5, katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Read More »

Ratiba ya Mazishi ya Mzee Kingunge Hii Hapa

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru enzi za uhai wake. RATIBA  ya mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, iliyotolewa na familia yake jana inaonyesha atazikwa leo Jumatatu katika shughuli itakayoanza saa 9:30 hadi 11:30 katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Taarifa hiyo iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati maalum ya shughuli hiyo, Omary Kimbau, inaonyesha kwamba mwili wa marehemu ...

Read More »

NHIF TANGA WAENDELEA KUHAMASISHA MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA

Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia Shabani kushoto akitoa elimu ya mpango wa Toto Afya kadi kupitia kipeperusi kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao kwenye viwanja vya Tangamano ambapo walikuwa wakihamasisha mpango wa Toto Afya kadi Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia Shabani ...

Read More »

NAIBU WAZIRI WA MADINI BITEKO ATATUA MGOGORO WA LESENI YA MADINI ULIODUMU KWA MIAKA KUMI MKOANI SHINYANGA

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia mamia ya wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana Februari 3, 2018. Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya uchimbaji baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa ...

Read More »

ASAS: CCM ITAWASHUGHULIKIA WATENDAJI WOTE WA SERIKALI WATAKAOKWAMISHA JUHUDI ZA RAIS DK. MAGUFULI

MJUMBE wa Halmashauri kuu  CCM Taifa (NEC ) Salim Abri amesema kuwa CCM Mkoa wa Iringa itahakikisha inamshughulikia  mtendaji yeyote wa serikali  atakayeonyesha dalili ya kukwamisha  juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli. Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa mwiki  alipokuwa akiongea na wananchma wa CCM Manispaa ya Iringa katika maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM ,alisema ...

Read More »

RAIS MAGUFULI AWATAKA VIONGOZI WA DINI NA WAUMINI WAO WASIJIHUSISHE NA MIGOGORO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi na waumini wa madhehebu ya dini nchini kujiepusha na migogoro ambayo imekuwa ikiharibu sifa na heshima ya taasisi hizo muhimu katika jamii. Mhe. Rais Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 04 Februari, 2018 mara baada ya kuhudhuria Ibada ya kuwekwa wakfu kwa Askofu wa Tano wa ...

Read More »

RC WANGABO AAGIZA WAKAMATWE WOTE WALIOCHOMA NA KULIMA MSITU WA MALANGALI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu akiwasilisha taarifa ya msitu wa Malangali uliopo Sumbawanga Mjini Kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa agizo la kukamatwa kwa waliokiuka amri ya mahakama na kufanya shughuli za kibinadamu kwenye msitu wa Malangali Mjini Sumbawanga katika Mkutano wa hadhara.    Mkuu wa mkoa wa ...

Read More »

RC Wangabo Awabaini Wakwepa Kodi Atoa Siku 7 Wajirekebishe Kabla ya Msako

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim wangabo amesikitishwa na kitendo cha wafanyabiashara kutumia mbinu mbalimbali za kukwepa kulipa kodi serikalini jambo linalorudisha nyuma maendeleo, hivyo kutoa siku saba za kujirekebisha kabla ya Mamlaka ya mapato kuanza msako mkali na kuwatia nguvuni. Amesema kuwa katika kipindi cha mitatu kuanzia Oktoba hadi Disemba, 2017 Mamlaka ya Mapato Rukwa imekusanya shilingi bilioni ...

Read More »

ZITTO KABWE AWATAKA CHADMA KUSITISHA KAMPENI JIMBO LA KINONDONI

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kupitia kwnyw kurasa wake Twitter amewataka CHADEMA kusitisha kampeni za Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa heshima ya Mzee Kingunge Ngombali Mwiru aliyefariki juzi hospital ya Muhimbili alipolazwa baada ya kung’atwa na Mbwa wake. Zitto Kabwe amesema CHADEMA wanapaswa kusitisha Kampeni mpaka Mzee huyo atakapozikwa, mzee Kingunge alikuwa na mwanachama wa CHADEMA baada ya kukihama ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons