Nyundo ya Wiki

Fahamu kuhusu ‘mwuaji’ watoto Njombe

Ni baba wa watoto wanne, mganga wa jadi aeleza siri imani ya utajiri wa kichawi Maisha ya mtuhumiwa, Joel Nzuki, katika kesi ya mauaji ya watoto watatu wa familia moja yameelezwa kutokuwa na viashiria vya wazi kwa mhusika kuhusishwa na unyama huo, JAMHURI limeelezwa. Kwa mujibu wa ndugu wa mtuhumiwa huyo, pamoja na wenzake wanaofanya biashara ya kuuza mbao pamoja ...

Read More »

Mjomba amtia mimba mpwawe (2)

Wiki iliyopita Gazeti la JAMHURI liliandika habari kuhusu binti wa shule anayedaiwa kutiwa mimba na mjomba wake. Hapa chini ni mwendelezo wa mahojiano ya wahusika wa tukio hilo. Endelea… Saimoni anasema kisa hicho kimetengenezwa na mama yake mzazi ili kukwamisha suala la mirathi, anasema familia yake wameamua ‘kumbambikia’ tuhuma hiyo kama njia ya kumficha mtuhumiwa halisi aliyetajwa kwa mara ya ...

Read More »

Mjomba amtia mimba mpwawe 

Ukishangaa ya Musa…hivyo ndivyo naweza kusema kuhusu binti (jina limehifadhiwa kwa sababu za kisheria) mwenye umri wa miaka 16, ambaye anatakiwa kuwa shuleni, lakini haiko hivyo kwake, yupo nyumbani analea mtoto wake mwenye umri wa miezi minne. Anatamani kupata nafasi ya kusoma tena lakini anashindwa kuwatumikia ‘mabwana wawili’, yaani mtoto na shule, yeye amechagua kumlea mtoto. Mtoto wake amepewa jina ...

Read More »

Mfugaji ‘atapeliwa’ mamilioni

Mkuu wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Luis Bura, kwa kushirikiana na Ofisa Mifugo na Mtendaji wa Kata ya Kifula wilayani humo wanatuhumiwa kumtapeli mfugaji wilayani humo kiasi cha Sh milioni 12. Mfugaji anayedai kutapeliwa anaitwa, Subi Gagi (56), ambaye ni mfugaji na mkazi wa Kijiji cha Ilunde, wilayani Kibondo, mkoani Kigoma. Gagi ameliambia Gazeti la JAMHURI kwamba Machi 5, ...

Read More »

Benki M yaikuza Benki ya Azania

Ukosefu wa ukwasi wa kutosha uliokuwa unaikabili Benki M umesababisha mali na madeni yake kuhamishiwa katika Benki ya Azania Ltd, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema. Uamuzi huo umefikiwa baada ya BoT kubaini kuwa benki hiyo imetetereka na kujikuta ikiwa chini ya kiwango cha ukwasi unaohitajika kwa mujibu wa sheria za benki wa Sh bilioni 15, kiwango ambacho kinatakiwa kulinda ...

Read More »

Jiji lanyang’anywa maegesho

Serikali imemkabidhi Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mkoa wa Dar es Salaam jukumu la kukusanya mapato ya maegesho ya magari kuanzia Februari mwaka huu. Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi George Tarimo, ameliambia Gazeti la JAMHURI kwamba mchakato wa zabuni ya ukusanyaji wa mapato ya maegesho ya magari bado unaendelea.  Mhandisi Tarimo amesema wanasubiri ...

Read More »

Aliyetekwa arejeshwa kwa staili ya Mo

Raymond Mkulo (29) anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana Novemba 18, mwaka jana katika ufukwe wa Coco, Dar es Salaam, naye amerejeshwa kwa mtindo unaoshabihiana na ule uliotumika kumrejesha mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo). Mkulo alipotea kwa siku 47 tangu alipotekwa akiwa kwenye gari lake aina ya Noah lenye namba T 961 DCJ. Gari hilo ndilo linalodaiwa kukodiwa na watu wawili waliotaka ...

Read More »

Sera ya uzazi wa mpango ibadilishwe

Septemba 9, mwaka huu Rais John Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi akiwa Meatu mkoani Simiyu aligusia uzazi wa mpango. Baada ya kuona, kusikia na kusoma mitazamo na maoni ya watu mbalimbali juu ya hoja aliyoitoa Rais Magufuli, nimeona nami nichangie mawazo kidogo juu ya hili; na kwa kweli kukazia maarifa juu ya kile alichokisema na mtazamo wake thabiti kwa masilahi ...

Read More »

GMO yafyekelewa mbali

Wananchi wadau wa kilimo wameupokea kwa shangwe na nderemo uamuzi wa serikali wa kupiga marufuku majaribio ya uhandisijeni yanayofanyika kwenye vituo vya utafiti nchini. Novemba 21, mwaka huu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe, aliiagiza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kusitisha mara moja utafiti huo nchini kote.  Uhandisijeni, yaani Genetic Modified Organism (GMO), ni utafiti ...

Read More »

Mchati: Mti wa thamani unaotoweka Mafia

Licha ya ukweli kuwa uoto wa asili wa Kisiwa cha Mafia unafanana kwa kiasi kikubwa na uoto wa asili wa visiwa jirani vya Pemba na Unguja na maeneo ya Bara yaliyopo jirani kama Kisiju na Rufiji, watafiti Rogers na Greenaway (1988) waliokuwa wakidurusu uoto wa Kisiwa cha Mafia walishangazwa mno na kiwango kikubwa cha upekee (endemism) wa mimea ya kisiwa ...

Read More »

Barua ya wazi kwa Rais wa Tanzania

Je, GMOs ni Sera ya Serikali? Mheshimiwa Rais; Kwa heshima na taadhima, niruhusu mimi mtoto wa mkulima mdogo na mwananchi wa nchi yetu tukufu nikusalimu. Hali yangu mimi na wanafamilia wenzangu, ambao ni wakulima wadogo nchini, si njema kabisa. Mheshimiwa Rais, kama ujuavyo, sisi ni takribani asilimia zaidi ya 70 ya wananchi wote, na naamini kuna ndugu zako wa damu ...

Read More »

Polisi aiba, aumbuliwa

Askari Polisi wa Wilaya ya Kinondoni amefanya uporaji kwenye ofisi za kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam. Oktoba 3, mwaka huu saa tatu usiku, askari aliyefahamika kwa jina moja tu la Shuka, akiwa na wenzake wawili walifika kituo cha mabasi Ubungo na kuwakamata wafanyakazi wa kampuni tatu za mabasi kisha kuwaweka chini ya ulinzi katika ...

Read More »

Rashid Malima sasa yametimia

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza kumsaka aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kukuza Maendeleo Vijijini (PRIDE Tanzania), Rashid Malima. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, John Mbungo, amesema Malima (65), anakabiliwa na tuhuma za kuchota Sh bilioni 1.8 ambazo ni mali ya PRIDE. Habari za kufilisika kwa PRIDE zilianza kuandikwa kwa undani zaidi na JAMHURI kuanzia toleo ...

Read More »

IGP Sirro usitishe wakosoaji, safisha Polisi

Nimesikiliza kauli ya Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro, kuhusu kupatikana kwa Mo Dewji. IGP Sirro amesema pamoja na mengi mengine kwamba wanaotafuta uadui na Jeshi la Polisi wasije wakalaumu litakapowatokea la kutokea. Kwake yeye, kukosoa utendaji wa Jeshi la Polisi katika masuala makubwa kama utekaji nyara wa raia ni kukosa uzalendo. Amehoji uraia wetu wote ambao tumekosoa sana utendaji ...

Read More »

Tanzania itajengwa na wenye moyo!

SIMULIZI YA KATIBU MUHTASI WA MWALIMU NYERERE   Jumamosi, Oktoba 22, 1966, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine jijini waliandamana kwenda Ikulu wakiwa na mabango yaliyoandikwa maneno machafu dhidi ya Serikali ya Awamu ya Kwanza iliyoongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Bango moja liliandikwa: “AFADHALI WAKATI WA MKOLONI.” Desemba 9, 1961 nchi yetu ilipata Uhuru ...

Read More »

MWANZA NA MWANDISHI WETU   Wanafunzi 12 wa Sekondari ya Igokelo, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, wamegundulika kuwa na ujauzito mwaka huu, hivyo kulazimika kuwa kando na masomo yao. Mimba hizo zimewalenga zaidi wanaosoma kidato cha kwanza, cha pili, tatu na nne walio na umri chini ya miaka 18. Mbali na na hayo, imegundulika pia baadhi ya wanafunzi wengine wa ...

Read More »

Serikali ‘isiwaue’ wafanyabiashara Kariakoo

NA MWANDISHI WETU DAR ES SALAM Wiki iliyopita kimefanyika kikao baina ya jumuiya ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo na mawaziri watatu; Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Charles Mwijage; Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe. Kikao hicho kimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam huku ...

Read More »

Jaji anyang’anywa jalada la mauaji Moshi

Na Charles Ndagulla, Moshi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Aishiel Sumari, amenyang’anywa jalada la kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Scolastica, Humphrey Makundi (16), JAMHURI limebaini. Hatua hii imekuja siku chache baada ya JAMHURI kupata taarifa za kiuchunguzi zenye kuonyesha kuwa Jaji Sumari alikuwa analalamikiwa, gazeti likachapisha taarifa ...

Read More »

Moyo wa hisani unatupiga chenga Watanzania

Majuma mawili yalilopita nilishiriki hafla ya kuchangisha pesa za hisani iliyofanyika Ojai, kwenye Jimbo la California nchini Marekani. Ni hafla inayoandaliwa kila mwaka na Global Resource Alliance, shirika lisilo la kiserikali linalosimamia utekelezaji wa miradi ya kusaidia jamii mkoani Mara. Ojai ni mbali. Nimeanza safari Alhamisi na kufika Jumamosi. Kwa ndege, siyo kwa basi la Zuberi. Siyo rahisi kusafiri zaidi ...

Read More »

Uhuru wa habari uanzie kwenye vyumba vya habari

DODOMA. EDITHA MAJURA. Serikali na Vyombo vya habari, wametuhumiana kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini. Wakati serikali ikituhumiwa kutofanya vizuri katika kudhibiti usalama wa wanahabari wanapotekeleza majukumu yao, serikali nayo imesema vyombo vya habari vinaminya maslahi ya wanahabari kiasi cha kusababisha washindwe kutekeleza majukumu yao kwa weledi unaohitajika. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akijibu ...

Read More »

Ndugu Rais, amani kwanza mengine tutayapata kwa ziada

Ndugu Rais, lengo la maandiko yetu siku zote siyo kukosoa. Udhaifu wa kuandika kwa sababu unampenda mtu au unamchukia mtu, Mwenyezi Mungu katuepusha nao. Hatuandiki kwa ushabiki wa kumshabikia mtu au chama fulani. Wala hatuandiki hapa kwa lengo la kusifia au kupongeza. Tunaandika kile ambacho tunaamini kuwa ni ukweli mtupu, kwa lengo la kushauri tu. Tunaamini kuwa kwa hizi busara ...

Read More »

Uvunjaji Chako ni Chako wageuka kitanzi DODOMA

EDITHA MAJURA Imebuka sintofahamu kubwa kutokana na uvunjaji wa jengo la Chako ni Chako mjini Dodoma, baada ya kuwapo harufu ya eneo hilo kuviziwa na “wakubwa”, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imevunja jengo lililokuwa maarufu kwa jina la Chako ni Chako, ambalo kwa miaka mingi limekuwa likitumiwa kwa biashara ya kuuza nyama ya kuku waliochomwa – ‘Kuku choma’. ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons