Siasa

Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi Yaja

Serikali ipo katika mchakato wa kuwashirikisha wadau ili kufikia azma ya kupeleka bungeni muswada wa sheria ya kulinda taarifa binafsi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Maria Sesabo, amesema. Sesabo amesema hayo mjini Dodoma wiki iliyopita, wakati wadau wa mawasiliano wakipewa ufafanuzi kutoka kwa wataalamu wa wizara hiyo, kuhusu mapendekezo ya kutungwa sheria hiyo. Kwa mujibu wa ...

Read More »

Nampongeza Rais Kurudisha Uwajibikaji

Namshukuru sana Rais John Magufuli kwa kurudisha uwajibikaji. Mimi ni mzee mwenye umri wa miaka 94 nikiwa miongoni mwa askari tuliopigana vita ya KAR ya mwaka 1952, namba yangu ilikuwa A.181300135. Malkia wa Uingereza alituma fedha za fidia lakini hatujalipwa hadi sasa. Hassan Sudai, Dodoma,0742082319, 0684820477 Mhariri wa JAMHURI Umesema ukweli Mhariri, kuna dalili zinazoashiria nchi hii kurejea katika mfumo ...

Read More »

Miaka 44 Gerezani

Ni mfungwa wa aina yake nchini. Ameingia gerezani vyama tawala vikiwa ni Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shiraz (ASP). Chama Cha Mapinduzi kimezaliwa mwaka 1977 akiwa gerezani. Amewekwa gerezani wakati ambao Tanzania haikujua kama itapigana na Uganda kwenye vita iliyokuja kujulikana baadaye kama ‘Vita ya Kagera’ (mwaka 1978-1979). Wala hakuona vita ya uhujumu uchumi ilivyoendeshwa na hayati Edward Sokoine. ...

Read More »

CCM Ijitenge na Siasa Huria

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetahadharishwa kujiepusha na hulka ya kuwapokea wanachama wanaotoka Upinzani, badala yake kijikite katika siasa za ukombozi zinazogusa ustawi wa maisha ya watu. Mhadhiri katika Idara ya Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ali, ametoa rai hiyo alipokuwa akihojiwa na JAMHURI mwishoni mwa wiki iliyopita. Mahojiano hayo yalihusu mwendelezo wa wanasiasa wakiwamo ...

Read More »

UWT ‘Ilivyomkuna’ JPM Wakati UVCCM Ikimsononesha

Mikutano ya uchaguzi kwa jumuiya mbili za Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanyika mkoani Dodoma wiki iliyopita, yote ikihutubiwa na Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli. Jumuiya ya Wanawake (UWT) ikafanya mkutano wa uchaguzi uliomchagua Gaudencia Kabaka kuwa Mwenyekiti, wakati Kheri James akichaguliwa kuiongoza Jumuiya ya Vijana (UV-CCM).     Hata hivyo, mkutano wa UWT ndiyo uliodhihirika kumfurahisha zaidi Rais Magufuli, ambaye hakuficha ...

Read More »

Ndugu Rais Tumeipuuzia Asili Aasa Tunawayawaya

Ndugu Rais, Tanzania kama sehemu nyingine ya Afrika tulikuwa na mambo mengi sana ya asili ambayo tumeyatelekeza baada ya wakoloni kuja kutuamulia yapi tuyaendeleze na yapi tuyatupe kabisa. Ni kweli sikumbuki ni lipi la asili ambalo wakoloni walituachia wakitutaka tuliendeleze. Mambo yetu mengi na hasa ya kitamaduni yalionekana ni ya kishenzi tu. Na sisi bila kudadisi ushenzi wetu ni nini ...

Read More »

Tusiwasahau Wapalestina

Juma lililopita Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza uamuzi wa serikali yake kuhamisha ubalozi wa nchi hiyo Tel Aviv kwenda Jerusalem. Ni hatua inayotokana na tamko kuwa serikali yake imetambua rasmi kuwa Jerusalem ni makao makuu ya Israel. Ni hatua inayochochea kudhoofika kwa jitihada za Wapalestina za kutafuta haki wanayoisaka tangu mwaka 1947. Kwa upande mmoja, unaweza kusema kuwa Rais ...

Read More »

Hakuna Uzalendo wa Hiari

Namwona Deodatus Balile kwenye Malumbano ya Hoja (ITV). Anajitahidi kueleza, lakini inshangaza sana baadhi ya wasemaji kunadi kuwa uzalendo ni suala la hiari!  Heee, ajabu sana! Uzalendo unajengwa tena kwa gharama kubwa -tutake tusitake- siyo suala la mtu kuzaliwa na kusema kwa hiari yake atakuwa mzalendo no way. Watawala wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kujenga fikra za kizalendo ndani ya ...

Read More »

Antonio Guterres ni nani?

Ni wazi sasa Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno, Antonio Guterres, ndiye Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa. Anatarajiwa kuanza kazi rasmi  Januari 2017 Katibu Mkuu wa sasa, Ban Ki-moon atakapomaliza muda wake. Kwa sasa, kiongozi huyo anasubiri kuthibitishwa rasmi na nchi wanachama wa Umoja huo, baada ya kupata uungwaji mkono wa asilimia 100 kutoka katika nchi wanachama wa ...

Read More »

Tusisahau historia hii (4)

Kwa wale wazee wenzangu nadhani kama bado wanakumbuka vile vijarida vya Sauti ya TANU, vilikuwa vinatuhabarisha mengi siku zile. Kwa mfano Sauti ya TANU na. 18 ya Desemba 16, 1957 ibara ile ya 5 Mwalimu Nyerere alisema wazi wazi kwa nini alijiuzulu nafasi yake ya kuteuliwa katika lile Baraza la Kutunga Sheria (Legico). Dai lake lilikuwa Baraza likubali kubadili Kanuni ...

Read More »

Barua ya kiuchumi kwa Magufuli

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, nakusalimu kwa salamu za heshima. Salamu hizi zinakujia kutoka kwangu mwananchi mwaminifu kwa nchi yangu ambaye nimeamua kukupa mkono wa shirika katika eneo la kuujenga uchumi. Baada ya salamu hizo ninatumia mwanya huu kukupongeza kwa kufanikiwa kupenya na hatimaye kuwa Rais, katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa sana ...

Read More »

Tuhoji mpango mpya wa maendeleo wa UN

Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa umezindua mpango mpya wa maendeleo na wa kupambana na umaskini duniani kufuatia kufikia tamati kwa Mpango wa Maendeleo ya Milenia. Mpango huu mpya unajulikana kama Sustainable Development Goals, na umepitishwa na viongozi wa nchi wanachama za Umoja wa Mataifa waliokusanyika New York kwenye kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Taarifa juu ya Mpango ...

Read More »

Umamluki katika siasa

Neno mamluki limekuwa linatumika zaidi kwa askari wa kukodishwa hapa ulimwenguni. Wakati Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasherehekea mwaka wake wa tano tangu kuasisiwa kwake  Septemba 1, 1969, Amiri Jeshi Mkuu, Mwalimu Julius Nyerere, alitamka neno “MERCENARY” hapa nchini.   Hebu tujikumbushe kwanza alivyosema Amiri Jeshi Mkuu; “Askari wako wa aina mbili. Lakini ingawa nazungumza habari za ...

Read More »

UTAFITI: Vyuo vikuu kuna ‘mateja’

Matokeo ya utafiti uliofanywa na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini (DCC), umebaini kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu hasa vya Dodoma pamoja na baadhi ya askari polisi wa mkoa huo, wamekuwa watumiaji wakubwa wa dawa hizo. Mtaalamu kutoka DCC na mmoja wa watafiti wa mradi huo, Yovin Ivo Laurent, alieleza hayo hivi karibuni Dar es Salaam wakati akitoa matokeo ...

Read More »

Watanzania sasa tukatae kutawaliwa

Minyukano ya kutafuta uongozi nchini tayari imeshaanza. Tumeshuhudia ya kushuhudiwa, mitandao nayo ipo kazini usiku na mchana. Inashangaza kuona harakati za kutaka kuwatawala Watanzania ambao dalili zinaonesha kuanza kupevuka uelewa, zimeanza kujidhihirisha. Wanaotaka utawala wamejisahaulisha ahadi zao na matatizo ya wapiga kura, badala yake wameanza kuelekeza nguvu kubwa kwenye sakata la udanganyifu kwa wadanganyika, kwa kutumia vijisenti na vijizawadi visivyo ...

Read More »

CCM na utawala uliofitinika

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kujifunza au kimepuuza matokeo ya migawanyiko na anguko kwa serikali mbalimbali duniani ziliendekeza tawala za kiimla dhidi ya haki, utu na usawa. Anguko la tawala dhalimu zilizodumu madarakani kwa ubabe na kukosa nguvu za hoja zilizokataliwa na kuanguka kwa kishindo ambazo CCM, imeshindwa kujifunza kwa kujidanganya kuwa itatawala milele ni kama zile Zaire (sasa Jamhuri ...

Read More »

CCM yachomoa tena panga lake

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea malalamiko mengi juu ya ukiukwaji wa taratibu na kanuni kabla na wakati wa kura za maoni, hivyo sasa vikao vizito vya chama vinatarajiwa kufyeka wagombea watakaotiwa hatiani.  CCM ina utaratibu wa kukata majina ya makada wake wanaoshutumiwa kutoa rushwa na kufanya vurugu baada ya taarifa kufikishwa ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ...

Read More »

Yah: Mimi siasa basi, naomba kazi mpya

Ukisikia mtu mwenye mkosi katika maisha ya siasa basi ni mimi Mzee Zuzu, ninayeishi huku Kipatimo. Naishi maisha magumu sana tangu nchi hii ilipopata Uhuru hadi imekomaa kwa Uhuru wake. Nimepigana usiku na mchana tangu nikiwa barobaro hadi naingia utu uzima, na sasa machweo ya uzee sijabahatika kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi, alimaarufu balozi huku kijijini kwetu. Nimewaza mambo mengi ...

Read More »

Mabadiliko ni mapinduzi, ni mageuzi

Binadamu awe mtu mmoja mmoja, kundi la watu au jamii fulani  wanapenda mabadiliko lakini wanahofia mabadiliko yenyewe yatakuwaje. Muasisi au waasisi wa mabadiliko huwa na wasiwasi kuhusu hayo wayatakayo kama yatafaulu au laa.Kwa sababu hawana uhakika na matokeo yake. Watu wanapotaka mabadiliko lazima wapwe na sababu za msingi na makini za kutaka mabadiliko. Siyo kwa sababu tu wafanye hivyo kwa ...

Read More »

Umuhimu wa wagombea huru sasa umedhihiri

Kama unahitajika ushahidi kuwa upo umuhimu wa kuruhusiwa kwa wagombea huru ndani ya Katiba ya Tanzania, basi umejitokeza sasa baada ya matukio ya hivi karibuni yaliyomo ndani ya siasa za Tanzania. Tukio lililohitimisha ukweli huo ushahidi ni kuhama kwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kwa maelezo ...

Read More »

Lowassa: Anayejua Richmond Kikwete

.Wasaidizi wake wasema “Mzee sasa ana amani” NA WAANDISHI WETU Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, kwa mara ya kwanza amemtaja Rais Jakaya Kikwete ndiye anayefahamu kwa kina mkataba wa Kampuni ya Richmond uliosababisha nchi kupata hasara ya mamilioni. Lowassa anasema, “mamlaka ya juu” ukiachilia mbali yeye aliyekuwa waziri mkuu wakati huo mkataba ukisainiwa ilikuwa inajua kila hatua na kwamba ndiye ...

Read More »

Wilaya, majimbo si suluhu ya matatizo

Namshuruku Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia afya njema na amani. Ni vyema tukamshukuru Mungu kila wakati kwa sababu tunaendelea kuyashuhudia mapenzi yake mema kwetu. Pili, niombe radhi kwa sababu lugha ya Kiswahili ni ngumu, hivyo katika kuandika inawezekana nikakosea hapa na pale ingawa si nia yangu kufanya hivyo. Ikitokea ikawa hivyo, basi ni bahati mbaya na tusameheane kwa wale watakaokuwa wamekwazwa. ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons