Tunaandaa vichaa, maskini

Nadhani kutokana na dawa za kulevya kuzagaa kila pembe hapa Tanzania ni ishara tosha inayoonesha kukosekana kwa hekima na busara kwa vijana na kuandaa taifa lenye vichaa na maskini wa mawazo. SOTE tukatae hali hii na sheria ifanye kazi kunusuru mambo kuharibika zaidi hapa nchini.

Mpenzi wa JAMHURI na nchi yangu

0684 144 080

 

Pua ndefu dili Karagwe

Kama wewe ni mrefu na una pua ndefu usiende kuishi Karagwe kwa sababu utakamatwa na kuambiwa wewe ni raia wa Rwanda, utatiwa misukosuko hadi ujutie kuzaliwa. Pua ndefu Karagwe ni dili, ila kama wewe ni Mshona kutoka Zimbabwe karibu Karagwe hutaitwa mhamiaji haramu! Kwa kweli nchi yetu hatuko makini, ni aibu!

 

Pius Lugwisa, Karagwe

0717 443 737

 

EA Tuungane kikamilifu

Kama wabunge hawapendi makao makuu ya Afrika Mashariki yawe Arusha watafute sehemu nyingine siyo waanze kutangatanga huku na kule. Nadhani ifike mahali tuwe na dira ya kuungana kikamilifu japo kimchakato zaidi kama vile uhuru kamili wa wana Afrika Mashariki wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila passport na vinginevyo.

 

Mpenzi wa Gazeti Jamhuri

0765 441 474

 

Walimu wanyanyaswa Mvomero

Baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kuhojiwa na LAAC Agosti, mwaka huu, walimu walioajiriwa 2012 idara ya sekondari mishahara yao imezuiwa na Ofisa Elimu wa wilaya hiyo. Hizo ni mbinu za kujaribu kurudisha fedha zilizoibwa. Wameamua kuumiza walimu hao.

 

Msomaji wa JAMHURI, Mvomero

 

Polisi wasibambike watu kesi

Nina wasiwasi kuwa dhana ya Polisi Shirikishi Jamii haitawezekana hapa Tanzania. Ninasema hivyo kwa sababu baadhi ya askari polisi hawatendi haki, badala yake wamekuwa wakiwabambika watu kesi kwa nia ya kujipatia maslahi binafsi. Mamlaka husika zishughulikie kero hiyo.

 

Magutu wa Nyamongo, Tarime

0752 469 159

 

Rais usilazimishe suluhu

Rais wetu Jakaya Kikwete usiogope kiasi cha kutaka suluhu na majirani zetu waolazimisha migogoro. Wacongo wasiyo na hatia wanakufa, tuwanusuru kwa  kuwatawanya M23 na mizizi yao popote ilipo. Rais wangu usilazimishe suluhu kwa sababu tu wamejitoa kwenye Bandari ya Dar, acha woga wewe ni luteni kanali.

Emmanuel Kalenzi, Mbozi

0714 477 085

 

Mahakama isimtupie DPP lawama

Kauli ya mahakama iliyotolewa na Jaji Kiongozi ina walakini, anamtupia lawama DPP kwa makosa yanayofanywa na ofisi yake kwa kutofuata taratibu katika kufungua kesi za watuhumiwa wa dawa za kulevya. Mahakamani anawaachia waliokamatwa na dawa za kulevya, kisa DPP amekosea kuandaa mashtaka. Kosa la DPP linamwondolea mtu kosa?

 

Mahande, DSM

0757 594 168

 

Tusikumbatie sera za Wazungu

Tujifunze kutokana na historia. Wewe mtu mzima utafundishwaje kumchukia mwenzako? Mzanzibar amchukie Mtanganyika? Cha ajabu Waafrika tunaendeleza mikakati ya Wazungu; DIVIDE AND RULE. Umoja uliozaa Tanzania ni kielelezo cha kiu ya kuungana kwa Waafrika. Tulidai uhuru, una gharama zake, tusirudie matapishi ya Wazungu.

 

Msomaji wa JAMHURI

0765 441 474

 

 

 

 

 

1320 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!