Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Aprili 13, 2026, amefanya mazungumzo na Balozi wa Slovakia nchini, Mhe. Ivan Lančarič, katika ofisi yake iliyopo Bungeni jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi, pamoja na kupanua wigo wa ushirikiano kati ya Tanzania na Slovakia katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zimekubaliana kuendeleza na kuimarisha ushirikiano katika sekta za uchumi, elimu, teknolojia, nishati na uwekezaji.








