Mwenyekiti CCM ashiriki Kongamano la Muungano Tunguu, Zanzibar
JamhuriComments Off on Mwenyekiti CCM ashiriki Kongamano la Muungano Tunguu, Zanzibar
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kikao pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya kushiriki kwenye Kongamano la Muungano lililoandaliwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Chuo cha Umoja huo kilichopo Tunguu, Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2026.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kuhusu Kiwanda cha Uchapishaji cha Chuo cha Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichopo Tunguu, Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2026.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye Kongamano la Muungano lililofanyika katika Chuo cha Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tunguu, Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2026.Viongozi mbalimbali waliopitia Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wakiwa kwenye Kongamano la Muungano lililofanyika katika Chuo cha Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tunguu, Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2026.