Na Mwandishi Wetu, Kinondoni

Mnamo Aprili 29, 2026 Mfanyabiashara Aliasgher Akhter Khakoo ambaye hufanya shughuli za usafirishaji mizigo na abiria alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani au kulipa faini ya Tsh. 3,000,000/= na kurejesha kiasi cha Tshs. 60,000,000/= alizojipatia kwa njia ya udanganyifu.

Katika shauri namba 15378/2025, Mshtakiwa Aliasgher Akter Khakoo alishitakiwa kwa kosa la kuwasilisha hundi benki ili aweze kupatiwa fedha huku akijua kuwa akaunti yake haikuwa na fedha hiyo. Mshitakiwa alisomewa shitaka la kurusha kishada (Kite Flying) kinyume na kifungu cha 332(B)(1) na (3) vya Sheria ya kanuni ya adhabu (Penal Code) Sura ya 16 Rejeo la 2022.

Mshitakiwa alipatikana na hatia kwa kosa hilo na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani au faini ya Tsh. 3,000,000 na mshitakiwa alilipa faini.

Shauri hili liliendeshwa na waendesha mashtaka wa TAKUKURU Kinondoni, Bw.Aidan Samali na Bi.Stella Mwengwa.