Na Francisco Peter, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Taasisi ya Education Malaysia Global Services wameamua kuja hapa nchini na kutangaza vyuo vikuu kutoka nchini Malaysia ili Watanzania wapate fursa ya kupata elimu kwenye vyuo bora duniani.

Katika kupata elimu vyuo bora taasisi hiyo imewashauri Watanzania kufika katika hoteli ya Serena siku ya leo kwa ajili ya kuona mapinduzi ya elimu ya vyuo vikuu mbalimbali kutoka Malaysia.

Watanzania wameshauriwa kulipa kipaumbele suala la elimu kwa kutembelea maonesho ya vyuo vikuu vya nchini Malaysia yanayofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es salaam.

Mmoja ya wanafunzi waliofika katika maonesho hayo Warida Ismail amesema kuwa kwa mwanafunzi aliyepata kusoma nje ya Tanzania hupo uwezekano mkubwa wa kutazamwa zaidi wakati wa fursa za kupata ajira mbali na kuwa amepata elimu nje ya nchi .

“Wanafunzi wenzangu wenye maono ya kupata fursa ya kwenda kupata fursa ya kielimu nje ya nchini wanaweza kuwa na faida zaidi ya kufanikisha kupata ajira mapema zaidi katika hali ya Ushindani wa soko la ajira mara wanapo kuwa wamemaliza masomo yao,” anasema Warida

Kwa upande wa mwanafunzi mwingine aliyefkka katika maonesho hayo Mikidadi Said amesema kuwa , “wanafunzi wa Tanzania tukipata fursa ya kwenda kwenye masomo wakajitume kwa bidii ilikuweza kufikia malengo ya mafanikio wanayoyataka”.

Wakati huo huo jana Juni 2,202 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elmu, Sayansi na Teknolojia, Daniel Mushi alikutana na wadau wakati wa kikao kazi baina ya vyuo hivyo vya Malaysia na wizara hiyo pamoja na vyuo vikuu wenza wa hapa nchini kilichoratibiwa na Taasisi ya Wakala wa Elimu Nje ya Nchi ya Global Education Link na kujadili masuala ya elimu.

Amesema lengo la kikao hicho kilikuwa na malengo ya kujadili kuelekea maonesho hayo ili kukuza mashirikiano baina ya Tanzania na Malaysia ambapo kimeandaliwa kwa uratibu wa Taasisi ya Global Education Link kwa ushirikiano na Taasisi ya Education Malaysia Global Services.

“Tumepata ugeni wa vyuo vikuu takribani tisa kutoka Malaysia na pia lengo ni kukuza fursa za mashirikiano na kama nchi tumeupokea ugeni huu kwa mikono miwili na kwenye majadiliano pia wameahidi kutoa fursa kwa wanafunzi wetu”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Education Link Limited,AbdulMalik Mollel ambao ni mawakala wa vyuo Vikuu nje ya Nchi amesema kwenye maonesho wameleta vyuo vikuu bora Duniani vyenye renki kubwa kutoka nchini Malaysia ambayo viko ndani ya vyuo hamsini bora Duniani.

Mollel amesema kupitia maonesho hayo ambayo yataanza asubuhi yatabeba lengo la ukuzaji wa elimu kwa vijana Watanzania na wataangalia namna vijana wanaweza kupata elimu ya chuo Kikuu ambapo mwanafunzi atasoma kwa miaka miwili hapa nchini na kisha kwenda kumalizia miaka iliyobaki katika vyuo vikuu nchini Malaysia.

Amesema Pia wataangalia jinsi wanafunzi kutoka Malaysia wanaweza kuja kusoma hapa nchini sambamba na kushauri vyuo vikuu vya Malaysia kufungua kampasi za elimu hapa nchini.

“Tunawaona wenzetu ni wanasayansi tena bora Duniani je tunaweza kuungana na wanasayansi wetu na wa kwao ili wanasayansi wetu waanze kuonekana kwa kupitia ushirikiano huu”amesema

Aidha kwa upande wake mratibu mwenza wa maonesho hayo Bi Esther Low ambaye pia ni afisa mkuu wa masoko na mahusiano wa taasisi ya Education Malaysia Global Services amesema wameamua kuja hapa nchini na kutangaza vyuo vikuu kutoka nchini Malaysia ili Watanzania wapate fursa ya kupata elimu kwenye vyuo bora Duniani, huku akiwakaribisha watanzania kufika katika hoteli ya Serena leo kwa ajili ya kuona mapinduzi ya elimu ya vyuo vikuu mbalimbali kutoka Malaysia.