Skip to main content

JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine
  • Home
  • Kitaifa
    • Biashara
    • Siasa
    • Uchumi
  • Kimataifa
  • Makala
    • Siasa
    • Uchumi
  • MCHANGANYIKO
  • Michezo
  • Burudani
  • Kazi/Ajira
  • Gazeti La Jamhuri
    • Sitanii
    • JAMHURI YA WAUNGWANA
    • Nyundo ya Wiki
June 8, 2018
Kitaifa

Jeshi la Zima Moto Yapewa Tuzo ya Heshima

Jamhuri Comments Off on Jeshi la Zima Moto Yapewa Tuzo ya Heshima

JESHI la Zimamoto na Uokoaji limepokea tuzo ya cheti cha heshima kwa kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji hapa nchini kutoka katika Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo.

 

Tuzo hiyo imepokelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Dar es Salaam.

 

Akizungumza Kamishna Jenerali baada ya kupokea tuzo ya cheti hicho alisema, anaishukuru taasisi hiyo kwa kulipa Jeshi hilo tuzo hiyo kwa kazi nyingi ambazo taasisi hiyo imezifanya kwa kushirikia na Jeshi hilo ikiwepo kampeni ya kuitangaza namba ya simu ya dharura 114.

 

Andengenye, amezitaka taasisi nyingine kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzifufua Fire Hydrant zilizo haribika na zilizofukiwa ili kuongeza idadi ya vifaa hivyo ambayo ni msaada mkubwa wakati wa majanga ya moto. ‘‘Jamii ishirikiane na Jeshi letu katika kuvilinda visima hivyo (Fire Hydrant) vilivyopo mitaani kwani ni msaada mkubwa pale majanga ya moto yanapotokea’’.

 

 

Ni vyema sasa mamlaka zinazoshughulikia miundombinu ya maji safi kwenye miji na majiji ikazingatia wanapotengeneza miundombinu hiyo, wakumbuke kuweka na mifumo ya maji ya zimamoto Fire Hydrant, pamoja na kuhakikisha wamiliki wanaojenga majengo makubwa na madogo wanaweka mifumo hiyo ya maji.

 

Tuna changamoto kubwa kwa upande wa visima hivyo, kwa hiyo kampeni yetu ya kufufua na kuongeza visima hivyo vitasaidia kuleta tija katika utendaji kazi katika fani yetu. Tunashirikiana na Mamlaka za Maji kuhakikisha miundombinu hiyo inarudi na kutoa ushauri pale miradi mipya ya maji inapo jengwa.

 

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania, Muhammad Shaban alisema wamechukua uamuzi huo wa kutoa Tuzo hiyo kutokana na kuona mchango mkubwa wa Jeshi hilo walioutoa katika jamii. Pia amesema wataendelea kutoa ushirikiano na Jeshi hilo katika utoaji elimu kwa umma. “Tupo tayari kushirikiana na Jeshi hili kuwaonesha sehemu zote ambazo fire hydrant zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam.”

 

“Kampeni ya kufufua fire hydrant imetugusa sana na kuona hatua hiyo ni msaada mkubwa kwa jamii kwani zitasaidia magari ya zimamoto na uokoaji kupata maji eneo la karibu majanga ya moto yanapotokea.”

Post Views: 552

Share this:

  • Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Share on X (Opens in new window) X

Like this:

Like Loading...
JESHI LA ZIMA MOTO
Previous Post Makundi ya Timu 16 Ligi ya Timu za Vijana Zatajwa
Next Post Viatu havibani, havipwayi vinatosha Na Angalieni Mpendu “Kweli nimeomba nipumzike kwa sabab
Posted By

Jamhuri

  • Mkurugenzi wa Uchaguzi apongeza ufanisi na uwazi wa mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja
  • Mwenge waingia Tanga, miradi ya bilioni 27 kuzinduliwa
  • Serikali yaimarisha usimamizi miradi ya umwagiliaji kuongeza uwajibikaji, ufanisi na thamani ya fedha
  • Waziri Kikwete : Utumishi wa Umma ni nguzo ya kufanikisha Dira ya Taifa 2050
  • Wananchi wavutiwa na elimu ya vipimo wanapata kuwa mabalozi wa WMA

Habari mpya

  • Mkurugenzi wa Uchaguzi apongeza ufanisi na uwazi wa mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja
  • Mwenge waingia Tanga, miradi ya bilioni 27 kuzinduliwa
  • Serikali yaimarisha usimamizi miradi ya umwagiliaji kuongeza uwajibikaji, ufanisi na thamani ya fedha
  • Waziri Kikwete : Utumishi wa Umma ni nguzo ya kufanikisha Dira ya Taifa 2050
  • Wananchi wavutiwa na elimu ya vipimo wanapata kuwa mabalozi wa WMA
  • Masoko ya Madini yaimarisha uwazi, kudhibiti utoroshaji
  • Umoja wa kitaifa ni muhimu katika utekelezaji wa Dira 2050 – Waziri Sangu
  • Ndege agawa kompyta, meza, kabati kwa shule na zahanati Babati
  • OWM yashiriki Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026
  • TANESCO muongeze vituo vya kuchajia vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme -Ridhiwani
  • Tanzania yazindi kupata uwekezaji kutoka mataifa ya nje
  • Marekani na Iran wasaini makubaliano ya kumaliza vita
  • Wachina wanne washindwa kusomewa mashtaka kwa kukosekana mkalimani
  • Wizara ya Viwanda na Biashara yahimiza vijana kutumia fursa za kiuchumi
  • Dk Katunzi awaalika wadau kusherehekea Jubilei ya dhahabu ya TBS

Copyright 2025

Designed by JamhuriMedia
%d