Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema Serikali imekamilisha maandalizi ya mkutano mkuu wa wanahisa wa Africa50 na jukwaa la miundombinu kwa asilimia kubwa.

Chalamila amesema mkoa umejipanga vyema, kuhakikisha mkutano unakuwa na utulivu na wananchi kuendelea kulinda amani.

Amesema mkutano huo ni muhimu sana kwetu na unatarajiwa kuhudhuliwa na watu zaidi ya 1200 kutoka ndani na nje ya bara la Africa.

Amesema mpaka leo kuna baadhi ya Marais, wanaweza kushiriki katika mkutano huo ni Rais wa Jamhuri ya Angola, Senegal, Msumbiji, Nigeria na Gabon.

Mkutano huu ni moja ya majukwaa makubwa zaidi, yanayolenga kujadili namna ya kurahisisha maendeleo ya miundombinu barani Africa kupitia ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma .

Amesema mkutano huo utatoa fursa azimu kwa Tanzania kama kitovu cha biashara ,uwekezaji na maendeleo ya miundo mbinu barani Africa kuwasilisha miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Reli ya kisasa yaani kwa maana ya SGR bandari ya Dar es Salaam miradi ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme pamoja na miundo mbinu ya TEHAMA

Ikiwa na lengo la kuwavutia wawekezaji wa kimataifa na kuharakisha utekelezaji wa malengo au ule mpango wa nne wa maendeleo ya taifa kwa miaka mitano
pamoja na dira ya taifa ya maendeleo ya taifa.

Napenda kuchukua nafasi hii, kuwahakikishia wananchi na wageni wote kuwa ,maandalizi yote muhimu yamekamilika kwa ushirikiano wa wizara mbalimbali taasisi za serikali vyombo vya vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wadau wote ili kuhakikisha mkutano huu unafanyika katika mazingira salama na tulivu ,,Amesema

Kwa upande mwingine Chalamila amewataka wananchi , kuendelea kuitunza na kuilinda amani kama nyenzo muhimu kuu ya diplomasia ya kimataifa na diplomasia .

Aidha amewahimiza wafanyabiashara wote na watu wa huduma wa sekta binafsi, kutumia fursa hii muhimu katika kutoa huduma bora zenye weledi uadilifu na zinazokidhi viwango vya kimataifa lakini si kwa vitendo vya kupandisha bei

Chalamila amesema Serikali inaamini kuwa mafanikio ya mkutano huo, yataongeza fursa za uwekezaji na kuitangaza zaidi nchi kukuza uchumi wetu kwa kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa pamoja na kufungua ajira na fursa mpya za maendeleo kwa watu wote