Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amewasili wilayani Songwe, mkoani Songwe, kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Iganjo mkoani Mbeya hadi Saza mkoani Songwe, pamoja na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Saza.
Kabla ya hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Mhe. Salome ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songwe na kufanya mazungumzo na uongozi wa Wilaya hiyo ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Fadhil Nkurlu.
Katika hafla hiyo, Mhe. Salome ameambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu; Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Simon Songe; pamoja na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Mhandisi Edson Ngabo.
Wengine ni wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na watendaji wa shirika hilo.










