Na Francisco Peter,Dar es Salaam
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na uongozi wa Chuo hicho jana kuhusu mafunzo ya bandari lengo kuu ni kuzalisha rasilimali watu bora kwa kuzingatia ujuzi, maarifa na mtazamo.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo hicho Dkt.Lufunyo Hussein amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa sasa wanaendelea na mipango ya kuimarisha mafunzo na kuongeza idadi ya wataalamu wenye uwezo na ushindani katika sekta ya bandari na uchukuzi ambapo inaendelea kutekelezwa kwa hatua mbalimbali, kuanzia uboreshaji wa miundombinu ya mafunzo hadi matumizi ya mifumo ya kisasa ya uigaji (simulators).
“Baada ya kukamilisha mipango ya sasa katika chuo kilichopo Dar es Salaam, kutafikiria namna ya kusogeza huduma zaidi katika matawi mengine kulingana na ukuaji wa sekta ambapo kwa sasa, madarasa yapo katika maeneo mbalimbali ya bandari ikiwemo Mtwara, Tanga, Kigoma na Mwanza, ambapo mafunzo ya muda mfupi hutolewa huko na walimu huenda kutoa mafunzo hayo, huku mafunzo ya vitendo yakifanyika kwenye bandari.
Dkt.Lufunyo amesema katika maelezo ya kiufundi kuhusu vifaa vya mafunzo, alibainisha kuwa kuna mashine tano zinazoweza kuwekwa na kuwafanya wanafunzi wafanye mazoezi ya vitendo, zikiwemo Harbour Mobile Crane (inayojulikana kwa uzoefu kama Gotwald), RTG (Rubber Tyred Gantry Crane), na RMG (Rail Mounted Gantry Crane).
Kwa upande wake mwalimu Franco Mwakatage ameelezea upande wa Simulator Buildin Short Couse ambapo
amesema kupitia mifumo hiyo, mwalimu hukaa katika kituo maalum (instructor’s station) kusanifu kazi, huku mwanafunzi akipewa mazingira tofauti ya uendeshaji kama vile mvua, mazingira ya usiku yenye taa, au upepo, ili kujenga umahiri katika mazingira mbalimbali.
Huku akieleza Mfumo wa full mission simulator huonyesha uwezo wa mwanafunzi , ikiwemo iwapo amegonga, anacheza, au kutoa viashiria vya mazingira halisi.
Pamoja na kuelezea masuala ya maendeleo katika chuo hicho chuo kinaendelea na mradi wa ujenzi katika upomradi unaoendelea ambapo unatarajiwa kukamilika ndani ya takriban miaka miwili (huku uhalisia ukitajwa kuwa miezi 18), na utawezesha kuwa na chuo chenye mazingira bora zaidi.




