• Yaibua maswali sita ya kisheria, yataka Mahakama ya Rufani kupitia uamuzi
  • Yahoji ushahidi wa uchochezi, kifungo cha miaka minne na siku 577 za mahabusu

Na Pendo Nguka, JamhuriMedia, Dar es Salaa

Hukumu iliyompeleka gerezani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeibua mjadala mpya wa kisheria.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaainisha maswali sita yanayogusa ushahidi, haki ya kujitetea na uhalali wa adhabu ya miaka minne.

Katika ripoti yake ya mwisho ya ufuatiliaji wa kesi hiyo, THRDC imehoji namna Mahakama Kuu ilivyomwachia Lissu huru dhidi ya shtaka la uhaini, lakini ikamtia hatiani kwa kosa la uchochezi ambalo halikuwa sehemu ya mashtaka ya awali.

Mtandao umetaka hoja hizo zichunguzwe katika ngazi ya rufaa, ukisisitiza kuwa mamlaka ya mahakama kumtia mshtakiwa hatiani kwa kosa dogo linalohusiana na shtaka kuu lazima yatumike bila kuathiri haki yake ya kupata taarifa za tuhuma na kuandaa utetezi.

Lissu alikabiliwa na shtaka la uhaini lililotokana na hotuba aliyoitoa Aprili 3, 2025, katika mkutano wa kisiasa uliozungumzia uchaguzi, mageuzi ya mfumo wa uchaguzi na haki za kisiasa.

Kwa mujibu wa taarifa ya THRDC, alikaa mahabusu kwa siku 577 kutokana na shtaka hilo kutoruhusu dhamana.

Novemba 6, 2026, Mahakama Kuu ilimwachia huru dhidi ya shtaka la uhaini, lakini ikamtia hatiani kwa uchochezi na kumhukumu kifungo cha miaka minne jela.

Uamuzi huo umeifanya THRDC kuibua hoja zinazohusu tafsiri ya sheria, kiwango cha ushahidi na namna haki za mshtakiwa zilivyolindwa katika mwenendo wa shauri.

Maswali sita

Hoja ya kwanza inahusu matumizi ya Kifungu cha 319 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambacho THRDC imesema kilitumika kumtia Lissu hatiani kwa kosa dogo baada ya shtaka la uhaini kutothibitishwa.

Mtandao huo umeeleza kuwa sheria inaweza kuruhusu mshtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa dogo linalojumuishwa katika shtaka kuu, lakini matumizi ya mamlaka hayo yanahitaji kuzingatia viini vya makosa na haki ya kujitetea.

KWA HABARI ZA KNA ZAIDI SOMA GAZETI LA JAMHURI LA NOVEMBA 24 – 30, 2026