JamhuriComments Off on Dkt. Tax akutana na Rais mstaafu wa Msumbiji
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chisano jijini Dar es Salam.
Dkt. amemshukuru Chisano kwa kukubali mwaliko wa kuja kushiriki utoaji wa Tuzo za Taifa za Uandishi Bunifu za Mwl. Nyerere zilizofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Aprili, 2023.
“Chisano naomba nichukue nafasi hii kukushukuru kwa kitendo cha kukubali kuja nchini na kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo uliofanyika jana, tunakushukuru sana na karibu tena Tanzania,” amesema Dkt Tax.
Amesema kitendo hicho kinaonesha uhusiano wa kidugu na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Msumbiji na pia kunaongeza jitihada za kuitangaza lugha ya Kiswahili katika bara la Afrika na Duniani kwa ujumla