Na Mwandishi Wetu, JAMHURI MEDIA

Klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia imeweka ofa ya kuvunja rekodi ya pauni milioni 259 kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe.

Nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa na Nyota Mshambuliaji katika Klabu ya PSG Kylian Mbappe 24

Nahodha huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye kandarasi yake, amekataa kusaini mkataba wa nyongeza katika klabu ya mabingwa hao wa Ufaransa na hakuwa sehemu ya kikosi cha ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini Japan.

PSG wanataka kumuuza Mbappe sasa kuliko kumwacha aondoke bure msimu ujao wa joto.

Uhamisho wa Neymar wa £200m kutoka Barcelona kwenda PSG mwaka 2017 ndio unaoshikilia rekodi ya sasa.

By Jamhuri